Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu

TIMU ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 wa Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao Yanga katika mchezo wa utangulizi uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa timu hizo mbili ambao ulikuwa wa utangulizi kabla ya mechi ya timu ya Simba na Yanga wanaoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Mtangane ulianza saa nane mchana ambapo vijana hao kwa kila timu walionesha umahiri wao wa kusakata kabumbu licha ya umri walionao. Timu ya vijana wa Simba walianza kupata bao la kwanza katika kipindi cha kwanza.

Kadri muda ulivyosonga ndivyo kila timu ilivyokuwa ikiusoma mchezo wa mpinzani na hivyo kipindi cha kwanza hadi kinakwisha  Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0 huku timu ya vijana wa Yanga wakionekana kutafuta bao la kusawazisha.

Dakika 45 za kipindi cha pili zilianza kwa kasi kubwa kwa kila  timu kuhakikisha inapata matokeo mazuri. Umaridadi wa pasi na ubora wachezaji wa timu hizo kulisababisha mashabiki wa soka waliokuwa uwanjani kushuhudia vipaji ambavyo vikiendelezwa na kutunza vitakuwa na tija kwa Taifa letu la Tanzania.

Hata hivyo kadri mpira ilivyokuwa kuendelea wachezaji wa Simba walionekana kupiga hesabu za kuhakikisha wanaongoza bao wakati kwa Yanga wakiwa na mkakati wa kusawazisha na ikiwezakana kuongeza na mengine.Timu ya vijana wa Simba walifanikiwa kupata bao la pili baada ya kugongeana pasi za uhakika .

Hivyo hadi dakika 90 za mchezo huo wa utangulizi zinamalizika timu ya Simba ya vijana wameibuka na ushindi wa mabao hayo 2-0 na kusababisha mashabiki wa Simba uwanjani hapo kufurahia matokeo hayo.

Mashabiki wa Simba ambao wameujaza upande wao wote katika  Uwanja wa Taifa walikuwa wakitoa tambo za kwamba ushindi ambao wamepata vijana hao ni dalili njema katika mchezo wao wa saa 11 jioni.

Wakati huo huo baada ya kumaliza kwa mchezo wa timu za vijana wa Simba na Yanga ,yalifuata mazoezi ya kwa wachezaji wa Simba na Yanga ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...