Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imezindua wimbo maalum wenye lengo la kuhamasisha Wanataaluma kujiunga na Bodi hiyo sambamba na kutoa elimu kwa umma kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Godfred Mbanyi amesema wimbo huo umejikita zaidi Wanataaluma kujisajili na Bodi na kufanya Mitihani ya Bodi na kubobea zaidi katika Taaluma hiyo.

Mbanyi amesema wimbo huo umetoa ujumbe mahsusi wa majukumu, kazi ambayo Bodi imepewa katika kuongeza ufanisi wa majukumu hayo kuongeza tija katika dhima ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda.

“Wimbo huu tutaufanyia uzinduzi katika Matamasha ya Vyuo na Shule mbalimbali katika Makongamano ya Wataalamu baada ya janga hili la Corona kupungua au kuondoka, pale ambapo Serikali itakapotoa ruhusa ya mikusanyiko tutafanya uzinduzi katika Vyuo vinavyotoa taaluma ya Ununuzi na Ugavi”, amesema Mbanyi.


Wimbo huo unapatikana katika Mitandao ya Kijamii ya Bodi hiyo (PSPTB) katika Tovuti (https://www.psptb.go.tz/) na Instagram (psptbofficial), Facebook (Bodi Ununuzi) na YouTube (PSPTB TV).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) , Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua wimbo wa Bodi hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...