WOTE kote duniani hivi sasa wanapambana na tatizo la ugonjwa wa Coronavirus. Serikali zote barani Afrika kwa namna mbalimbali zinapambana kuhakikisha maambukizi hayasambai.

Tanzania nako hali ni hiyo hiyo. Hatua mbalimbali zimechukuliwa kupunguza mikusanyiko mfano kufunga mashule na kuzuia mikutano ya hadhara na michezo. Hata watu binafsi nao wanabadili mwenendo wao wa maisha kuwa kupunguza idadi ya watu wanaokutana nao.

Sekta ya biashara nayo vivyo hivyo. Baadhi ya hoteli zimesimamisha huduma kwa muda kupunguza uwezekano wa maambukizi huku sekta ya kilimo ikizidisha nguvu kuhakikisha chakula kinapatikana. Ama kwa hakika, ugonjwa huu umeonyesha namna sekta mbalimbali zimejiunga pamoja kukabiliana na adui na uzoefu huu utasaidia sana ziku zijazo hasa katika kufanya maamuzi ya kijamii na kibiashara.

Kwa mfano inafahamika wazi kwamba kampuni ya Tigo nchini Tanzania iko katika hatua za kuorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam baadaye mwaka huu jambo ambalo lingewezesha umma kununua hisa hizo, swali linabaki kwamba, mlipuko huu wa ugonjwa huu utalazimu kuchelewa kwa hatua hiyo chanya kwa sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania?

Wataalamu wa uchumi na biashara wanaeleza kuwa zoezi hilo huleta pamoja wadau katika mikutano mingi kulijadili kabla ya kukamilisha na kuongeza iwapo litacheleweshwa kutokana na janga hili vikao vya wadau kukutana uso kwa uso havitakuwepo msimu huu.

Nyakati hizi za sintofahamu tunapata faraja kwa habari chanya kuhusu tunapoelekea kama nchi na dunia nzima. Hata hivyo ni wakati sahihi pia wa kutofanya yale ambayo yanaweza kusubiri mpaka wakati sahihi lakini lengo iwe ni kusaidia umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...