Jana baada ya taarifa rasmi ya Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar - Mhe Hamad Rashid Mohamed kuelezea kuwa wamepata wagonjwa wawili wa Corona wote wakitokea Tanga, tayari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga na vyombo vya usalama vimefanya jitihada za ziada kuweza kuwabaini wagonjwa hao. 

Mmoja, ni mwanaume mwenye umri wa miaka 33 aliyeingia Zanzibar tarehe 18 March kupitia bandari ya Mkokotoni amethibitika kuwa ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Bushiri kutoka Wilaya ya Pangani. Wa pili, ni mwanaume mwenye umri wa miaka 27 aliyeingia Zanzibar tarehe 13 March kupitia bandari ya Mkokotoni amethibitika kuwa ni mfanyakazi wa moja ya Hotel Zanzibar aliyekuja Tanga mapumzikoni naye anatokea Kwediboma Wilaya ya Kilindi. 

Kwa mujibu wa taarifa ya wataalam wa afya ni kuwa wagonjwa hawa wamegundulika wakiwa na ugonjwa huu zikiwa zimezidi siku 14 toka kuwasili Zanzibar, hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa ugonjwa huu waliupata aidha wakiwa safarini kuelekea Zanzibar au baada ya kuwasili Zanzibar. Mhe Martine Shigela pamoja na vyombo vya usalama vya Mkoa na Wilaya zote mbili, tayari wameshatembelea maeneo husika na kuwabaini wale wote waliokuwa karibu na wahusika kabla ya safari na tayari watu hao wapo chini ya uangalizi wa madaktari kwa siku 14 ili kujiridhisha kabisa kuwa hawajaathirika na ugonjwa huo. Hata hivyo, hakuna mtu yoyote wa karibu aliyekuwa na dalili zozote zinazo ashiria ugonjwa huo. 

Mhe Martine Shigela amewataka wananchi wote kuepukana na mikusanyiko katika kipindi hiki, kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji yanayotiririka au sanitizer; na kuwataka wananchi waendelee kutoa taarifa kwa mgeni yoyote atakaye bainika kuingia katika Mkoa. Mpaka sasa wageni zaidi ya 140 wapo kwenye karantini katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa baada ya maelekezo ya serikali kuhakikisha wageni wote wanao ingia ndani ya nchi kwa siku 14 wakae karantini.

 Serikali ya Mkoa wa Tanga itaendelea kuchukua hatua za ziada kuhakikisha wananchi wake wanaendelea kuwa katika hali ya usalama na amani. Kwa pamoja kwa kufata maelekezo ya wataalamu wetu wa afya tunaweza kukabiliana na ugonjwa huu.

Imetolewa:
06/04/2020
Pangani, Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...