Katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 25, benki ya Stanbic Tanzania imezindua shindano la wajasiriamali kwa lengo la kuchochea ukuaji wa shughuli za kibiashara nchini Tanzania. Shindano hilo liitwalo, ‘Stanbic Entrepreneurship Challenge’ linatarajiwa kuanza tarehe 28 Mei hadi tarehe 11 Juni mwaka huu – ambapo washindi watano watazawadiwa shilingi milioni 10 kila mmoja.

“Nchini Tanzania, sekta ya biashara ina makampuni ya biashara ndogondogo na za kati (SMEs) zaidi ya milioni 3, ambazo zinamchango mkubwa katika kukuza na kuimarisha uchumi. Na kwa kuwa ni dhumuni letu kuu ni kuhakikisha kwamba sekta hii inakuwa, kwa miaka mingi tumekuwa tukiendesha programu ambazo zimeweza kuwanufaisha wajasiriamali kupitia mafunzo, kuwaunganisha wataalam wa biashara na kuwaandalia madarasa na wakufunzi sekta ya biashara”, alisema Mkuu wa Idara ya Masoko wa benki ya Stanbic, Desideria Mwegelo.

Shindano hili linawalenga wafanyabiashara ambao wanaweka jitihada kubwa kuhakikisha wanafikia malengo yao kupitia miradi inayoleta manufaa ya kijamii, kwenye sekta za afya, elimu, mazingira, teknolojia, pamoja na shughuli za uzalishaji na chakula. Miongoni mwa vigezo vya shindano hili ni kuwa washiriki lazima wawe wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Moshi na Dodoma. Maelekezo ya namna ya kushiriki shindano hilo yanapatikana katika tovuti na kurasa za mitandao ya kijamii za benki hiyo.

“Napenda kuwahamasisha wajasiriamali kujisajili na kutuma maombi yao ya ushiriki na kuufanya mwaka 2020 kuwa mwaka wa kutimiza malengo – kwa kuchukua hatua za kukuza biashara zao au kuimarisha kwa biashara zao baada ya kuathiriwa na janga la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19,” Aliongeza.

Mbali na kukabidhi fedha taslim, washindi hao watapatiwa ushauri wa kifedha na usimamizi kutoka kwa wataalamu wa masuala ya kibenki, pamoja na kupatiwa nafasi ya kuunganishwa na makampuni ya kibiashara ambayo yana ushirikiano na programu zenye kusaidia kuendeleza biashara ndogondogo na za kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...