Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewakutanisha Wakuu wa Vyuo Vikuu vyote  nchini  kwa lengo la kuweka mkakati wa pamoja wa namna ya kufikia malengo ya ufundishaji na ukamilishaji wa Mitaala pindi Vyuo vitakapofunguliwa Juni 1, 2020.

Akifungua kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara Ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema pamoja na mambo mengine  watakubaliana namna bora ya kuhakikisha vyuo vinafidia muda wa masomo uliopotea na kukamilisha mihula bila kuathiri taaluma.

Mengine yaliyojadiliwa katika  kikao hicho ni kuhakikisha vyuo vinawasilisha nyaraka zote muhimu ili wanafunzi wapate Mikopo yao mapema vyuo vitakapofunguliwa.

"Hakikisheni katika vyuo vyenu  mnachagua maafisa mikopo ambao watatoa ushirikiano mzuri kwa wanafunzi ili kusiwe na malalamiko wakati wa kushughulikia mikopo yao," alisisitiza Dkt. Akwilapo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Makamu Wakuu wa Vyuo, Marasi na Maprovosti Tanzania (CVCPT) ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda amesema wanaishukuru Wizara kwa kuitisha kikao hicho ili kuweka mipango kwa pamoja utakaowasaidia kufungua vyuo bila changamoto na kwamba vyuo tayari vimejipanga  kuhakisha Jumuiya za Vyuo zinakuwa salama dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuzingatia  maelekezo ya wataalamu wa afya huku wakiendelea na masomo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru amesema Bodi imejipanga kutoa mikopo kwa wanafunzi kwa wakati kwa kushirikiana na vyuo huku akivishauri vyuo hivyo kushirikiana na uongozi wa wanafunzi wakati wa zoezi la utoaji mikopo ili kurahisisha utekelezaji wa kazi hiyo.
 Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (wa nne kutoka kushoto)Manaibu Makatibu wakuu Prof. James Mdoe (aliyesimama kulia kwa Katibu Mkuu) Dkt Ave Maria Semakafu(kushoto kwa Katibu Mkuu)wakiwa kwenye picha ya pamoja  na wakuu wa Vyuo baada ya kikao cha kuweka mkakati wa pamoja kilichofanyika jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akiongea na Wakuu wa Vyuo vikuu nchini (hawapo pichani) katika Kikao cha kuweka mkakati wa pamoja wa namna ya kufikia malengo pindi vyuo vitakapofunguliwa
 Baadhi ya Wakuu wa Vyuo wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (hayupo pichani) wakati wa  ufunguzi wa kikao cha kuweka mkakati wa pamoja kuelekea kufungua Vyuo Juni 1, 2020 kilichofanyika jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Makamu Wakuu wa Vyuo, Marasi na Maprovosti Tanzania (CVCPT), Prof. Raphael Chibunda akitoa ufafanuzi wa mipango waliyoiweka ya kuwezesha kufungua vyuo bila changamoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...