Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashugwa akikagua bidhaa ya unga wa viazi lishe unaochakatwa na mashine kutoka SIDO na kampuni Ng’hami Industries Company Ltd iliyopo Maswa – Simiyu. Leo 30 juni 2020 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashugwa akipokea maelekezo ya mchato mzima wa uandaaji wa viazi lishe jinsi vivyochakatwa hadi kupata unga wa viazi lishe katika kiwanda cha Ng’hami Industries Company Ltd kilichopo Maswa – Simiyu. Leo 30 juni 2020
(Picha zote na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara)
…………………………………………………………………………………….
Na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafukuza kazi wafanyakazi wa shirika hilo wanaowatoza fedha na wanaochelewesha zoezi Kutoa nembo ya ubora kwa bidhaa zinazotengenezwa kwenye Viwanda vidogo nchini.
Waziri Bashungwa ametoa maelekezo  hayo leo 30 juni 2020 alipofanya ziara mkoani Simiyu na kutembelea kiwanda cha Usindikani wa Viazi lishe kilichopo wilaya ya Maswa kinachojulikana kwa jina la Ng’hami Industries Company Ltd.
Bashungwa amefikia maamuzi hayo baada ya kufika kiwandani hapo na kukagua bidhaa za kiwanda hicho ambayo ni unga wa viazi lishe na kugundua hazina nembo ya ubora ya TBS, ambayo changamoto hiyo imesababiswa na wafanyakazi wa shirika la TBS kwa kuwaomba fedha kwa ajiri ya kupewa nembo ya ubora pia kuchewesha kwa zaidi ya miezi saba bila kupewa  majibu au nembo ya ubora.
Waziri Bashungwa baada ya kuona changamoto hiyo alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa TBS na DKt. Yusuph Ngenya na kumuelekeza kuwafukuza kazi wafanyakazi wake wanaokwenda kinyume na maagizo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutowachelewesha wafanyabiasha kwa sababu ambazo sio za msingi zinazosababisha bidhaa kutopewa nembo za ubora kwa wakati ambazo zinasababisha mazingira ya Rushwa na usumbufu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Ntobi Rufunga ameeleza kuwa barua ya kuomba nembo ya ubora ilipelekwa TBS tangu mwezi 11, 2019 lakini mpaka sasa hajapewa majibu yoyote na baada ya  kuchukuliwa kwa sampuli ya bidhaa hiyo wameombwa kutoa kiasi cha Tsh. 520,000/= ili wapewe nembo ya ubora ambayo ni kinyume na sheria na mashariti ya  shirika hilo.
Aidha Bw. Ntobi  amesema kuwa Kiwanda hicho mpaka sasa kinazalisha unga wa viazi lishe wa aina mbili ambao ni Unga wa kupika uji kwa ajiri ya matumizi ya rika zote pia Unga wa kutengeneza keki, mikate na andazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...