Na Said Mwishehe,Michuzi TV
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt.John Magufuli ametumia mkutano wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama hicho kumuombea msamaha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhman Kinana ambapo kwa kauli moja wametangaza kumsamehe.
 
Akizungumza mbele ya wajumbe wa mkutano huo ambao wamekutana Dodoma kwa ajili ya kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo ya kupitisha jina la mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na jina la Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi Mkuu mwaka huu, Dkt.Magufuli alitumia nafasi hiyo kutoa ombi la wajumbe hao kumsamehe Mzee Kinana kwani alishaomba msamaha hadharani.
 
"Aliyekuwa Katibu Mkuu wetu Abdulrhman Kinana amesamehewa ametubu hadharani na ninyi wajumbe mmemsamehe hadharani, kokote huko aliko muda huu ajue CCM tumemsamehe ,na hakika amefanya jambo la ushujaa na heshima kubwa.Nishatoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa CCM kumualika Kinana ili kesho awepo kwenye Mkutano Mkuu yeye pamoja na viongozi wengine kwa ajili ya kushuhudia mafanikio ambayo tumeyapata nchini kwetu,"amesema Dk.Magufuli.
 
Awali wakati anamzungumzia Kinana, Dk.Magufuli alisema kuwa kuna makosa ambayo walibainika kuyafanya na Chama kikawajadili na baada ya kutoa onyo kwake , Kinana aliamua kujitokeza hadharani kuomba radhi miezi minne iliyopita, hivyo ameona ni vema leo akatumia mkutano huo kupenyeza ajenda hiyo kwa ajili ya kumsamehe.
 
Amefafanua Dk.Magufuli kwamba "Mzee wetu Abdulrahman Kinana amekiri hadharani kuwa alifanya makosa, ni uamuzi mgumu kukiri hadharani, Chama kiliamua kumpa adhabu ya miezi 18 na tayari ameshatumikia miezi minne, kwa hivyo ndugu wajumbe ninawaomba tumsamehe na kisha aje ajiunge nasi, lakini yule mwingine simtaji jina lake najua mnafahamu(Membe) amejitoa mwenyewe."
 
Amewashukuru wajumbe kwa kumsamehe mzee Kinana, binadamu wote tunakosea na Chama hiki kinachotaka ni watu kukubali makosa yao na kuomba msamaha, Kinana amefanya hivyo, ameonesha uungwana mkubwa.Tunamsamehe." 
 
Hata hivyo baada ya Kinana kusamehewa, Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa Dk.Magufuli alianzisha wimbo mbele ya wajumbe hao kwa kuimba hivi "Tunaimani na Kinana....oyaa oyaa...tunaimani na Kinana oyaa oyaa ...Kinana kweli ...kweli...kweliii...kweli kweli kweli Kinana."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...