ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)Joshua Nasari ametangaza kukihama Chama hicho na  kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Nasari ambaye ameweka rekodi ya kuwa mbunge aliyeiingia Bungeni akiwa na umri mdogo kuliko wote amefikia uamuzi huo wa kujiunga na CCM leo Julai 8,2020 ambapo ameeleza ametafakari sana na kuona Chama sahihi kwake ni CCM.

Akifafanua zaidi  mbele ya wanachama wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Arusha Zolothe Steven, Joshua Nasari  amesema sasa iko mbegu ambayo aliiotesha na hatimaye leo imesimama mbela ya wana CCM.

Amefafanua ameamua kwenda CCM sio kwasababu anataka kugombea ubunge bali amefanya hivyo baada ya kutafakari kwa kina , kushauriwa na familia,ndugu ,jamaa na marafiki,hivyo akaona ni vema akajiunga CCM .

"Wameniambia hapana,wazee wa Meru wameniambia hapa,hivyo nimekuja CCM, huwa Wameru tunamsemo wetu kuwa unapokunywa maziwa lazima uangalie yanatoka kwa ng'ombe wa rangi gani,mweupe,mwekundu au mweusi.

"Hivyo nimeungana na ninyi ili Watanzania wanywe maziwa bila kujali yanatoka kwa ng'ombe wa rangi gani.Nimekuwa mbunge kwa term mbil,sio term moja,msinione mdogo na ndevu zangu chache ,nimekuwa mbunge kwa awamu mbili wa kuchaguliwa,"amesema Nasari na kuongeza yeye ndio mbunge mdogo kuliko wote.

Amesisitiza inawezekana wana CCM hawakuwahi kusema lakini roho zao ni mashahidi kwamba hakuwa mbunge lele mama ,na kama kufanya kazi basi aliwafanyia wananchi wa jimbo lake kwa kiwango kikubwa.

"Sasa swali la kujiuliza kama nilikuwa mtoto ,na nikakoswakoswa na kila aina  ya mabalaa,sio kwamba sikuwa naiona CCM,nilikuwa naiona .Hata nilipokuwa mbunge baada ya kumalizika kwa term ya kwanza ningeweza kujiunga CCM lakini nikasema hapana bado,"amesisitiza.

Nasari amesema huko nyuma akiwa Mbunge alizungumza sana kuhusu ardhi, na suala la ardhi kwao ni la kihistoria na watu wa Meru ni jambo ambalo limekaa moyoni, walifukuzwa kwa nyumba zao kuchomwa moto wakati wa Ukoloni maeneo ya Ngarenanyuki.

"Mwaka 1949,1950 na mwaka 1951, watu walichomewa nyumba zao na Wakaloni wakasema tutawapeleka kokote ilimradi tubaki na ardhi hii,"amesema Joshua Nasari ambapo hakusita kueleza kuwa katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 alijua kabisa hatashinda,hivyo hakuona sababu ya kupoteza muda wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...