Na Shukrani Kawogo, Njombe

Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Njombe Erasto Ngole ametoa onyo kwa mwanachama yeyote wa chama hicho atakayepinga jina la mgombea litakaloteuliwa na vikao halali vya uteuzi atafukuzwa uanachama mara moja.

Hayo aliyasema katika mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Ludewa na kuongeza kuwa kwa sasa kila mtia nia ana kundi lake ambalo linamshabikia kitu ambacho kinaruhusiwa kwa kila mwanachama kuwa na mgombea wake lakini baada ya uteuzi makundi yote yanapaswa kuvunjwa na kumuunga mkono mgombe atakayepitishwa.

Alisema wanachama wote wanatakiwa kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha kuwa mgombea atakayepitishwa na kamati hiyo anapata ushirikiano wa kutosha kwa wanachama na si kuendeleza makundi ambayo yanaweza kusababisha mvurugano katika chama.

“Mtu asikupangie mgombea unayetakiwa kumshabikia kwakuwa kila mtu anamgombea wake anayemtaka lakini kosa kubwa ambalo linaweza kukufanya ufukuzwe uanachama ni kupinga jina la mgombea litakaloteuliwa na vikao halali vya uteuzi hivyo ole wako wewe utakayepinga jina hilo maana utafukuzwa asubuhi tu! na hii ni amri ya kamati kuu”. Alisema Ngole.

Wakati huo huo mkutano huo ulihusisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho ambapo katika utekelezaji huo umeonyesha kuwa na mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali.

Akitoa ripoti ya miundombinu ya barabara injinia wa TARURA wilayani Ludewa Bujene Jilala alisema kuwa mtandao wa barabara uliopokelewa mwaka 2017 ukiwa na urefu wa kilometa 784.01 na kuongezeka kwa kilometa 256.36 zilizo nje ya mfumo na kuwa barabara rasmi za TARURA na kupelekea kuwa na mtandao wenye urefu wa kilometa 1040.37.

Aliongeza kuwa kilometa 9.5 ya mtandao wa barabara ni kiwango cha lami (DBSD), kilometa 225.32 ni bara bara za changalawe na kilometa 810.5 ni barabara za udongo ambapo kilometa 218.35 zipo katika hali nzuri, kilometa 549.13 zipo katika hali ya kuridhisha na kilometa 272.87 zina hali mbaya.

Aidha kwa upande wa kaimu mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Thomas Kiowi alisema kwa kipindi cha miaka mitano miradi mingi imetekelezwa na serikali kuu pamoja na wadau wa maendeleo katika sekta ya afya, elimu, maji, kilimo na ushirika, mifugo na uvuvi pamoja na miundombinu ya barabara ambapo uwekezaji huo unakadiliwa kufikia shilingi 27,006,473,573.72 
 Katibu wa siasa na uenezi CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiongea na wajumbe wa Halmashauri kuu wilaya ya Ludewa. ( Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Ludewa Stanley Kolimba, Katibu CCM Ludewa Bakari Mfaume, Mbunge aliyemaliza muda wake Deo Ngalawa na  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Ludewa Andrea Tsere.)
 Wajumbe wa kamatu kuu ya CCM Wilaya ya Ludewa wakiwa katika ukumbi wa mkutano.
 Katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na chama
Baadhi ya viongozi wa chama wakijadili jambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...