BILIONEA Wa Tanzanite, Laizer Saniniu leo Julai 12 , 2020  ametembelea mabanda mbalimbali  kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam 

Akizungumza akiwa kwenye mabanda ya sabasaba amewataka wachimbaji madini wadogo wadogo wasibweteke na fedha kidogo wanazopata na kuwafanya waache kuendelea kuchimba madini na badala yake wanatakiwa kuendeleza jitihada za kuchimba na ipo siku wataibuka mabilionea.

Laizer akifafanua zaidi mbele ya waandishi wa habari katika banda la Tume ya Madini amesema kwamba "Mimi nimetokea familia ya hali ya chini, nimekuwa mvumilivu sana katika kazi hii ya uchimbaji madini.

Sikukata  tamaa kwa fedha ndogo ndogo nilizokuwa napata kutokana na uchimbaji, niliendelea kuchimba nikiamini ipo siku Mungu atanipatia mawe ya kunipa kipato kikibwa zaidi na kweli ndivyo ilivyokuwa." 

Ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali kwa kila hatua waliyochukua kwa ajili ya mchakato wa kupima madini yake na kisha kuyanunua na kumpatia fedha hizo kwa uaminifu. 

Hata hivyo ameziomba mamlaka husika zisiwanyaanyase wachimbaji wadogo kwani wengi wao ni masikini sana na wanategemea kazi hiyo iweze kuwainua kiuchumi pamoja na  familia zao.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...