Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika kwenye kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere Marehemu Balozi Job Lusinde aliyefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Msemaji wa Familia ya Marehemu Balozi Job Lusinde, Waziri Mkuu Mstaafu John Samweli Malecela wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Marehemu Balozi Lusinde Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mke wa Marehemu Balozi Job Lusinde, Mama Sara Lusinde aliyekaa katikati mwenye kilemba cheupe mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kutoa pole nyumbani kwa Marehemu Balozi Lusinde Uzunguni jijini Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wafiwa nyumbani kwa kwa Marehemu Balozi Job Lusinde Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Msemaji wa Familia ya Marehemu Balozi Lusinde, Waziri Mkuu Mstaafu John Samwel Malecela mara baada ya kutoa pole Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...