NA MWANDISHI WETU, SABASABA

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba amesema zaidi ya wanachama wapatao 826 wamehudumiwa na PSSSF kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam tangu yalipoanza Julai 1 hadi leo Julai 10, 2020.

Bw. Kashimba ameyasema hayo leo Julai 10, 2020 wakati alipotembelea viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam ambako ndiko kunakofanyika maonesho hayo yaliyopewa kauli mbiu isemayo “Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.

“Tuko katika banda namba 13 tuliloliandaa kwa ushirikiano na NSSSF kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanachama wetu, tunatarajia tutaendelea kuwahudumia wanachama zaidi hadi hapo maonesho yatakapofikia kilele chake, tunawakaribisha wanachama wetu na wananchi kwa ujumla. Hapa sabasaba tuna ofisi kamili .” Alisema Bw. Kashimba.

Alisema huduma zote zinazotolewa kwenye ofisi za PSSSF zilizoeneo nchi nzima zinapatikana kwenye banda hilo na kuwahimiza wanachama na wananchi kufika ili wahudumiwe.

“Mwanachama atapata huduma zote kama anataka kupata ufafanuzi kuhusiana na uanachama wake, kuhakiki taarifa zake, kuangalia michango yake na mambo yote yanayohusiana na uanachama huduma zinapatikana hapa.” Alisisitiza.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba (kushoto) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda la Muko katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba Julai 10, 2020. Katikati ni Afisa Habari Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi.
 mamia ya wanachama wakiwa kwenye banda la PSSSF
 Meneja wa PSSSF Mkoa wa Kinondoni, Bi. Ritha Ngallo (kushoto) akimuhudumia mwanachama
 Meneja wa PSSSF Mkoa wa Ilala, Bi. Uphoo Swai (kulia) akifurahi na mwanachama wa Mfuko Bw. Malima Ndelema wakati akimuhudumia kwenye banda la Mfuko.
 Mhasibu Mkuu wa PSSSF Mkoa wa Kinondoni, Bi. Rehema Gumbo (kushoto) akimuhudumia mwanachama.
 Bw. Kashimba akiwa na Bw. Njaidi kwenye banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambao nao wameshiriki katika maonesho hayo ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
 Bwa. Kashimba (kushoto) na Bw. Njaidi (mwenye t-shirt ya blue) wakibadiliahsna mawazo na baadhi ya wakurugenzi wa NSSF kwenye banda la ushirikiano namba 13 ambalo mifuko hiyo miwili inashirikiana.
 Bw. Kashimba akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha PSSSF kinachoendelea kuwahudumia wanachama wa Mfuko huo kwenye banda namba 13 maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa Sabasaba
Hili ndio banda namba 13.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...