Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA)  kimeendelea na utoaji wa ushauri kwa  wanafunzi wanaohitaji kujiunga na masomo katika chuo hicho kwa mwaka mpya wa masomo unaoanza Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na Michuzi Blog katika maadhimisho ya 44 ya maonesho ya Kimataifa Sabasaba kwa mwaka huu, Afisa Uhusiano mwandamizi Sarah Goroi amesema chuo cha IAA ni cha Serikali chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Sarah amesema, katika chuo banda lao ndani ya Viwanja vya Sabasaba wanatoa huduma za ushauri kwa wanafunzi wanaohitaji kujiunga kwa mwaka mpya wa masomo 2020.

Amesema, pia wanatoa uthibitisho kwa wale wanafunzi waliochanguliwa moja kwa moja na TAMISEMI pamoja na udahili kwa wale wanaojiunga na ngazi ya Certificate, Diploma, Degree na Masters katika kozi tofauti.

"Kwa mwaka huu tumeongeza kozi zingine mpya kuanzia ngazi ya Certificate hadi Masters na katika banda letu tunafanya udahili kwa wanafunzi wapya pamoja na wale waliomaliza Elimu ya kidato cha Nne na kuchaguliwa na serikali kwenda Vyuoni moja kwa moja," amesema Sarah.

Aidha, Sarah ameeleza kuwa mbali na masomo yanatolewa kwa wanafunzi walio watanzania na wasio watanzania,  Chuo cha IAA wanafanya tafiti mbalimbali .

Katika ngazi ya Certifcate, kozi tatu zimeweza kuongezeka ambazo ni Certificate in Library Studies and Information Science, Certificate in Insurance and Risk Management With Apprenticeship na Basic Technician Certificate in Business Management with Chinese

Ameongeza kuwa, kwa ngazi ya Diploma kozi zilizoongezeka ni nne ambapo ni Diploma  in Library Studies and Information Science na Diploma in Insurance and Risk Management With Apprenticeship, Diploma in Multimedia na Diploma in Strategies Studies.

Pia, kwa ngazi ya Bachelor Degree kozi tisa zimeongezwa kwa mwaka mpya wa masomo  na sita zikiwa kwa wale wanaohitaji kusoma ngazi ya Masters.

Sarah amewataka wananchi kutembelea banda lao kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo huduma ya elimu na kutoa ushauri kwa wanafunzi kuhusu kozi zinazopatikana kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha.
Afisa Udahili wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sekunda Titus akigawa vipeperushi na kutoa maelezo kwa watu waliotembelea banda lao ndani ya Maonesho ya 44 ya Sabasaba  yanayofanyika katika Jiji la Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof Eliamani Sedokeya akizungumza na Mkuregenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa Dkt. Elirehema Doriye alipotembelea banda la  Chuo cha Uhasibu Arusha katika maonesho ya 44 ya Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sarah Goroi  akigawa vipeperushi na kutoa maelezo kwa watu waliotembelea banda lao ndani ya Maonesho ya 44 ya Sabasaba  yanayofanyika katika Jiji la Dar es Salaam.
Afisa Udahili wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sekunda Titus akigawa vipeperushi na kutoa maelezo kwa watu waliotembelea banda lao ndani ya Maonesho ya 44 ya Sabasaba  yanayofanyika katika Jiji la Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mwandamizi Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sarah Goroi  akitoa maelezo kwa watu waliotembelea banda lao ndani ya Maonesho ya 44 ya Sabasaba  yanayofanyika katika Jiji la Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...