Wadau wa Sayasi, Teknolojia na Ubunifu wakiwa katika Kongamano lililofanyika katika maonesho ya Sa asaba jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuadhimisha siku ya Sayansi hapa nchini.
  Katibu mkuu wa wizara ya Elimj, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa mdahalo wa ulioandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TUME ya Sayansi na Teknolojia nchini (COSTECH) yaadhimisha siku ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa kuandaa kongamano la wadau wa sayansi pamoja na ubunifu katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.

Mdahalo huo umefanyika ili wananchi wanaotembelea katika maonesho ya biashara ya 44 kujipatia uelewa, kutoa mawazo yao pamoja na Kujielimisha masuala mbalimbali kuhusu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Kila ifikapo Julai 6 kila mwaka maadhimisho haya hufanyika ili kutoa uzoefu kwa watu wengine wenye bunifu mbalimbali kupeleka mawazo yao ubunifu katika Sayansi na teknolojia ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Katika Maadhimisho ya Mwaka huu kauli mbiu ni Utafiti na Ubunifu kama msingu wa Kukuza uchumi wa Viwanda kwa ajira na biashara endelevu.

Akizungumza katika Mdahalo huo, Katibu mkuu wa wizara ya Elimj, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema kuwa uzalishaji wa viwanda unategemea zaidi teknolojia ambayo inazalishwa hapa nchini kuliko teknolojia inatengenezwa nje ya nchi kwa itakuwa na gharama zaidi na inaweza isiendane na mazingira ya nchi yetu.

Maada zilizojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na i. Kubadilishana uzoefu unaotokana na ushiriki katika ubunifu na ujasiriamali, (ii) Mchango wa Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) katika kuchochea maendeleo ya sekta ya viwanda na (iii) Nini kifanyike kuwezesha sekta binafsi kuongeza ushiriki katika kuchangia maendeleo ya utafiti na ubunifu

Amesema kuwa leo la kongamano hilo ilikuwa ni kuangalia wabunifu wa kitanzania wanaweza wakatumika katika kuongeza uzalishaji katika nchi yetu na katika kukuza uchumi.

Amesema kuwa kila nchi inatumia wabunifu wa nchi yake katika kukuza uchumi pamoja na vipato.

"Ukitaka kupata teknolojia kutoka nje ya nchi utaipata kwa gharama kubwa na pengine isifae kwa mazingira uliyopo". Amesema Dkt. Akwilapo.

Amesema kuwa wafanya biashara, wakulima, watu wenye viwanda na wabunifu  lazima waungane ili kuongeza dhamani ya mazao hapa nchini ili  malighafi ipatikane kutoka hapa hapa nchini ili tuweze kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amosi Nungu, amesema kuwa lengo kuu la kufanyia mdahalo huo katika viwanja vya maonesho ya sabasaba ni kukutanisha watafiti, wabunifu, wagunduzi  na jamii ili kuangalia namna bora ya matokeo ya utafiti na ubunifu yanaweza kuifikia jamii.

Dkt. Nungu amesema kwa kuwa tupo katika uchumi wa kati ubunifu na viwanda vinahitajika zaidi ili kuweza kuzalisha bidhaa ambazo zitakidhi viwango vya kimataifa. 

Mbunifu George Buchafwe yeye ameongeza dhamani ya zao la Mchikichi pamoja na kupunguza muda wa kutengeneza mazao yatokanayo na mchikichi kwa kutumia teknolojia mbalimbali.

"Kwa upande wangu nimejikita zaidi kuongeza dhamani ya zao la Mchikichi ambalo kwa miaka ya nyuma lilikuwa halina dhamni yeyote."

"Kwa kutumia Ardhi tuliyonayo tunaweza kuzalisha Mchikichi na ikiwezekana kupanda mchini kama zao la nyumbani kama pambo wakati huo huo likawa linaongeza mapato." Amesema Buchafwe.

Amesema kuwa Kwa miaka mingi malighafi ya kuongeza dhamani zao la mchikichi imekuwa ikinunuliwa nchi za Ulaya lakini kwa sasa Teknolojia hiyo tunayo hapa nchini ambayo inatumika kuchakata zao hilo.

Licha ya hilo amesema kuwa ameshatoa mafunzo wa watu wengi na sasa zao la mchikichi linadhamani kubwa ukilinganisha na hapo awali.

"Tunashukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe magufuli kwa kuja na kauli mbiu ya Viwanda ambapo imetuwezesha kutupa hamasa ya kuendeleza  buhifu zetu."

Buchafwe amasema kuwa wananchi kwa sasa wanalima zao la mchinichi kwani wamepata soko, wameongeza kipato pamoja na Halmashauri zinakusanya ushuru kutokana na zao hilo.

Licha ya hili serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza zao la Mchikichi kuwa ni zao la kimkakati  kwani teknolojia za wazawa hapa nchini zimeweza kuongeza dhamani ya zao hilo.

Mwitikio wa Teknolojia yetu ni mkubwa kwani tumekuwa na viwanda 78 na baadhi ya Mikoa imeshaanza kupanda zao hilo kama Kyela, Morogoro, pwani, pamoja na Taasisi za serikali wameshaanza kupanda zao la Mchikichi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...