Serikali imewataka Watanzania kuwa wabunifu katika nyanja sayansi na teknolojia ili kukuza uchumi wa wa viwanda, ajira, biashara endelevu na uchumi.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia, Leonard Akwilapo katika majadiliano ya maadhimisho ya siku ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwl Nyerere (Sabasaba).

Majadiliano hayo yalishirikisha wadau mbalimbali ikiwa pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO), Sido, Veta, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na wengineo

Bw. Akwilapo alisema kuwa Tanzania ambayo kwa sasa ni miongoni mwa nchi zenye uchumi wa Kati, zinahitaji maelendeleo katika sekta ya viwanda na uzalishaji ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi.

Bw Akwilapo alisema kuwa Tanzania ina wabunifu wengi wa teknolojia, lakini wanashindwa kukuza kipato kitokana na kuzalisha bidhaa ambazo zinakosa masoko.

“Kuna wabunifu wengi sana katika masuala ufundi na teknolojia, lakini wengi wao wanakosa njia bora ya kuboresha kazi zao na kujikuta wanazalisha bidhaa ambazo zinakosa soko katika ushindani.

Kinachotakiwa hapa ni kuboresha bidhaa zao na kukidhi haja ya mlaji katika masoko ambako kuna ushindani wa hali ya juu, “ alisema Bw Akwilapo.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli inatilia mkazo maendeleo katika sekta ya viwanda ambayo itakuwa uchumi wanchi.

“Hivi sasa Tanzania ipo katika nchi zenye uchumi wa kati, ili ni jambo la kujivunia sana kwani nchi nyingi hazijafikia hapo,” alisema.

Katika majadiliano hayo, jumla ya mada kuu tatu zilijadiliwa zenye lengo la kuendeleza kukuza uchumi wa viwanda, kuongeza ajira na biashara.

Maada hizo ni kubadilishana unaotokana na ushiriki katika ubunifu na ujasiriamali, mchango wa matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifi ( STU) katika kuchochea maendeleo ya sekta ya viwanda na Nini kifanyike kuwezesha sekta binafsi kuongeza ushiriki katika kuchangia maendeleo ya utafit ina ubunifu.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu alisema kuwa majadailiano hayo yameleta tija kubwa kwa wadau na kuwa kichocheo cha maendeleo katika sekta hiyo na ubunifu.

Dkt Nungu alisema kuwa katika kuhakikisha sekta ya Teknolojia na Ubunifu inaendelea, Costech imeanzisha mashindano ya Kitaifa ya Sayansi , Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) ambapo yanafanyika kila mwaka ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha wanafunzi kuanzia shule ya Msingi mpaka vyuo kikuu na Costech imekuwa ikitoa fedha kwa washindi ambao wanahitaji kuboresha kazi zao za ubunifu.

Alifafanu kuwa mashindano yamekuwa na mafanikio makubwa ambapo mwaka jana kulikuwa na washindi 60 ambao ubunifu wao mbalimbali ulikubaliwa na kupewa msaada wa kuboreshwa ili kuongeza ajira na kipato.

“Mwaka huu kulikuwa na washindi 70 ambao kazi zao zimeshinda na jukumu lilolobaki ni kuhakikisha kuwa zinaboreshwa kabla ya kuanza kutumika katika soko la biashara,” alisema Dkt Nungu.

Alisema kuwa Costech imekuwa ikiwawezesha washindi kuanzia Sh600,000 na kuendelea kwa kutegemea mahitaji ya uboreshwaji wa kazi husika.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia, Leonard Akwilapo akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya Mwl Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam,Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu na pichani kati ni Mwenyekiti wa bodi ya sayansi na teknolojia Tanzania (COSTECH),Profesa Makenya Maboko.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia, Leonard Akwilapo akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya Mwl Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam,Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu na pichani kati ni Mwenyekiti wa bodi ya sayansi na teknolojia Tanzania (COSTECH),Profesa Makenya Maboko na kulia ni Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Maulilio Kipanyu.
Wa pili kulia ni ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya siku ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech),Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia, Leonard Akwilapo ,kulia ni Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Maulilio Kipanyula na pichani kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya sayansi na teknolojia Tanzania (COSTECH),Profesa Makenya Maboko pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu




Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wadau kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt Amos Nungu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu
maadhimisho ya siku ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya Mwl Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Baadhi wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...