Umoja wa viongozi wa kimila (MACHIFU) pamoja na Wazee wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya leo wamefika nyumbani kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na kumpatia pesa taslim ambazo wamezichanga kwa umoja wao ili ziweze kumsaidia kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo ambalo anatarajia kugombea kwenye uchaguzi mkuu 2020 ambalo hadi sasa hajalitaja.

 “Tumekuja kwa ajili ya kumtakia kila la kheri katika kule anakokwenda kugombea, sisi kama wazazi tumemkubalia na tunamtakia mafanikio mema huko anakotaka kwenda”

“Tunafahamu kwamba ametia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge, kikubwa kilichotusukuma kufanya hiki leo ni kutokana na jitihada kubwa alizozifanya na anazozifanya katika taifa letu kwenye maeneo mbalimbali”- Joel Mwakatumbula, Mkuu wa Machifu Rungwe

Kwa upande wake Dkt. Tulia amesema >>”Niwashukuru sana Wazazi wangu hawa kwa upendo mkubwa walionionesha pamoja na Baraka zao, ni wazi pengine ningeweza kupungukiwa hiyo pesa lakini wakaona mtoto wetu asijekuacha kuchukua fomu kwa kukosa hiyo pesa. Hakika wameianzisha safari ambayo na wao wameona ulazima wa kuwa sehemu ya safari hiyo” –Dkt. Tulia.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...