Na Said Mwishehe,Michuzi TV.

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Hussein Mwinyi amesema katika safari yake ya kisiasa kuna makundi mbalimbali ya waliomsaidia kufika hapo alipofika.

Miongoni mwa viongozi ambao amewashukuri ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye ndio alikuwa wa kwanza kwa kumuamini kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Afya.

"Mzee Mkapa naomba nimshukuru, nikiwa kijana wa miaka 33 aliniteua kuwa Naibu Waziri wa Afya, naomba nikishukuru kwa dhati, naomba nikishukuru hadharani leo hii.Hakuishia hapo hata uliopoanzia Taasisi ya Mkapa Foundation aliniteua kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa taasisi yake,"amesema Dk.Hussein.

Pia amesema anamshukuru Rais Mstaafu Jakaua Kikwete ambaye katika miaka yake yote 10 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne alimuamini na kumuweka kwenye Baraza lake la Mawaziri.

Dk.Hussein ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.Amesema kupitia Dk.Magufuli kuna mambo mengi ya uongozi amejifunza na yatamsaidia katika safari yake ya kuwatumikia Watanzania wote kwenye nafasi ya Urais.

"Miaka 11 nimekuwa katika Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  katika miaka mitano nimekuwa na Rais Magufuli, nimejifunza mengi kutoka kwako, wapo wanaosema mimi ni mpole, lakini nimejifunza rushwa, ufisadi, ubadhirifu, na uzembe vinataka ukali,hivyo nitakuwa mkali,"amesema Dk.Hussein Mwinyi.

Wakati huo huo amesema anamshukuru Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye ndiye mzazi wake.

"Napenda pia kumshukuru mzee Ali Hassan Mwinyi,namshukuru Mzee Mwinyi kwa kunilea, kama nina malezi mema basi yanatokana na malezi yake,"amesema.

Ametumia nafasi hiyo kumshukuru mama yake mzazi Mwasiti Mwinyi kwa malezi mema."Baada ya hapo nawashukuru wajumbe wa Kamati Kuu kwa kupitisha jina langu kuingia kwenye tatu bora na hatimaye Halmashauri Kamati Kuu ya CCM kunichagua kwa asilimia78.

"Tulikuwa wagombea  32 na hivyo wenzangu 31 wamebaki kuwa marafiki na wamenihakikishia kwa pamoja kuwa tutashirikiana kwa pamoja na kushinda.Sasa hakuna tena timu Mwinyi, tumebaki timu moja ya CCM.

"Katika tatu bora nilikuwa na Shamsi Vuai Nahodha na Dk.Mohamed Khalid,sisi na wengine wote tumekuwa wamoja.Hivyo wapambe tunaomba wote tuungane,"amesema Dk.Mwinyi.

Amesema jana baada ya kumaliza ,simu yangu ilikuwa inaita wakati wote kutokana na pongezi ambazo nimepata kutokana na hatua hii ambayo nimeifikia,niahidi ushirikiano mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...