Na  Ashura Mohamed -Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta amepiga marufuku kuegesha Magari katika  eneo la  wazi la bondeni badala yake Eneo Hilo  litatumika kama eneo la kupumzikia wananchi wote wa Arusha.

Akizungumza Mara baada ya kufanya ziara katika Eneo Hilo Kimanta alisema kuwa Eneo Hilo la wazi litatumika Kama bustani ya kupumzikia, wananchi kwa kuwa Ni Eneo ambalo linamilikiwa na Serikali.

"Eneo hili litatumika kwa ajili ya wananchi kupumzika na haya ni maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli siku aliyotuapisha”.

Aidha Kimanta amewata  wananchi ambao wanaegesha magari  katika eneo hilo kuondoa magari yao ifikapo Julai Mosi,2020 ili kuliacha eneo hilo wazi kwa ajili ya wananchi kupumzika baada ya shughuli zao za kila siku.

Amesema serikali inampango wa kuliboresha eneo hilo vizuri na kuwa la mapumziko kwa wananchi, kwani eneo hilo linamilikiwa na serikali na ni lawazi.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuaminiana kwa  kuwa mkoa huo,utajengwa na wanaarusha kwa maslahi mapana ya mkoa huo.

Nae mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini  Kenani Kihongosi alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Dkt.John Pima kuhakikisha kuwa Eneo Hilo halikusanywi Ushuru kuanzia July Mosi kutoka kwa mtu yeyote badala yake libaki kama lilivyo.

Kihongosi amelitaka jiji la Arusha kukaa chini na kuja na mpango mkakati ambao utaamua Eneo Hilo litafanywa Nini  ili wananchi waweze kupumzika na kulitumia.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.John Pima alisema kuwa amepokea maelekezo yote kutoka kwa mkuu wa wilaya na kuanzia July Mosi Eneo Hilo litafungwa na kufanyiwa marekebisho ili pawe pazuri na wananchi waweze kupumzika.

"Ninachoomba wananchi wa Jiji la Arusha mtuunge mkono ili tuweze kutekeleza yake ambayo mnatamani yawe hapa Arusha,kwa vitendo na kwa ushirikiano wa Pamoja"alisema Pima.
Kuanzia tarehe Mosi

Eneo hilo  lililopigwa marufuku kwa ajili ya  maegesho ya Magari lipo karibu na Msikiti wa Bondeni uliopo Jijini Arusha.
Pia Kimanta amefanya ziara fupi katika Jiji la Arusha na kukagua baadhi ya maeneo ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya 
Terrati.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Idd Hassan Kimanta amesema eneo la  wazi la bondeni litatumika kama eneo la kupumzikia wananchi wote wa Arusha Ameyasema hayo alipokuwa akikagua eneo hilo lilipo karibu na msikiti wa Bondeni jijini Arusha na kuzungumza na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo.
“Eneo hili litatumika kwa ajili ya wananchi kupumzika na haya ni maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli siku aliyotuapisha”.

Pia, amewataka wamiliki wa magari yote yaliyokuwa yameegeshwa katika eneo hilo la wazi kutumia eneo la wazi la Msikiti wa bondeni kuegesha magari yao kwa kufuata taratibu za eneo la Msikiti.
Picha na Woinde Shizza


 Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta katikati akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Kenani Kihongosi na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha dkt.John Pima.
Pichani mkuu wa wilya ya Arusha Mjini Kenani Kihongosi akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha dkt.John Pima akiwa wanapokea  Maelekezo katika baadhi ya Mradi katika Jiji la Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...