Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kujua changamoto zote zilizokuepo kwenye vyama vya ushirika kwenye mikoa yao.

Jafo amewataka wakuu hao wa mikoa pamoja na kujua madhaifu yaliyopo kwenye vyama hivyo pia watafute mikakati ya kuviimarisha lakini kuhakikisha kila chama wanakijua.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa pamoja wa wakuu wote wa mikoa nchini wenye lengo la kujadili Vyama vya Ushirika nchini, Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Oktoba mwaka juu na migogoro ya ardhi.

Akizungumza kwenye mkutano huo Jafo amesema mkutano huo utatumika kuwapa maandalizi wakuu wa mikoa kupokea vyama vya ushirika ambavyo vinaondolewa kutoka kuwa chini ya Wizara ya Kilimo na sasa vitasimamiwa na Ofisi ya Rais-Tamisemi.

" Tume ya Ushirika muda siyo mrefu sasa itakua ikifanya kazi na Wizara yetu ya Tamisemi ambapo nyinyi wakuu wa mikoa ndio mtakua wasimamizi wake kwenye mikoa yenu. Niwaombe mjiandae kuvipokea vyama hivi.

Nafahamu kuna mambo mlikua hamridhishwi nayo kwenye vyama hivi kwa sababu yalikua hayaendi vizuri na kwa sababu hamkua na mamlaka nayo mkawa mnashindwa kufanya maamuzi, sasa vyama hivi vinaenda kuwa chini yenu kwenye mikoa yenu mvisimamie vizuri viinuke na kuwa msaada kwa wananchi wetu," Amesema Jafo.

Amesema matamanio yake ni kuona sasa vyama vya ushirika vinaenda kuimbwa nchi nzima kwa sababu vitakua msaada mkubwa kwa wanachama wake na watanzania kwa ujumla.

"'Ofisi ya Rais-Tamisemi imefanya mambo makubwa kwenye usimamizi wa miradi mbalimbali ikiwemo Hospitali, Vituo vya Afya, Shule na miradi mingine, na nyie wakuu wa mikoa ndio mlikua wasimamizi wakuu sasa nataka kuona mkifanya hivyo huku kwenye vyama vya ushirika," Amesema Jafo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ameipongeza serikali kwa uamuzi wake huo wa kuishusha tume ya Ushirika Wizara ya Tamisemi kwani sasa itawafanya wakuu wa mikoa kuwa na nguvu kwenye vyama hivyo.

" Hakika haya ni maamuzi ya busara sana ambayo serikali yetu chini ya Rais Magufuli imeyafanya, na sisi kama viongozi wakuu wa mikoa tunaahidi kuvisimamia vyama hivi ili viweze kuwa msaada kwa wananchi na watanzania kwa ujumla," Amesema Mtaka.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza na Wakuu wa Mikoa katika mkutano wa pamoja wa kujadili maendeleo ya Vyama vya Ushirika ambapo sasa Tume ya Ushirika itakua chini ya Tamisemi badala ya Wizara ya Kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza na wakuu wa mikoa ambao wamehudhuria mkutano wa kujadili hali ya vyama vya ushirika jijini Dodoma leo.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambao wamehudhuria mkutano wao na Waziri wa Nchi-Tamisemi jijini Dodoma ambao umelenga kujadili hali ya vyama vya ushirika nchini
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...