Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv. 
 
Mbio za kuwania Jimbo la Nkenge Wilayani Missenyi kupitia CCM, zimemuibua Ndg. Thobias Mwesiga aliyewahi kushika nafasi ya pili katika Ngazi ya Uwenyekiti wa UVCCM-Taifa, ambae kwa sasa yupo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, na kumfanya kuvuta fomu ya kuwania Ubunge Jimboni humo Mkoani Kagera. 
 
Ndg. Thobias Kama Kada wa CCM amechukua fomu yake Julai 14 na kuirejesha Julai 15 akisindikizwa na mkewe. Tayari kwa kinyang'anyiro cha kuwania Kiti hicho.
 
 Ikumbukwe kuwa Ndg. Thobias amekuwa mwanachama wa 13 kurejesha fomu kati ya wanachama 45 waliovuta fomu hiyo ya kugombea nafasi ya ubunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...