Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya amemuagiza meneja wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula mkoa wa Njombe na Iringa NFRA  pamoja na mhandisi mkazi wa TBA kumsimamia mkandarasi anaye jenga maghala  mawili ya  kuhifadhi  chakula mjini Makambako na kutaka maghala hayo  kukabidhiwa mapema mwezi Disemba mwaka huu.
Kusaya amechukua  uamuazi huo baada ya mkandarasi anaye jenga maghala hayo kusuasua kukamilisha ujenzi ambao mpaka sasa ulitakiwa uwe umekamilika na kuanza kuhifadhi nafaka mbalimbali  jambo ambalo limekuwa kinyume na makubaliano ya mkataba.
“Chukueni hatua TBA tunachotaka ikifika disemba 31 mimi nije hapa tarehe moja mwaka 2021 mnikabidhi majengo yangu hicho ndicho tunachotaka”alisema Kusaya
Awali kaimu meneja wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula mkoa wa Njombe na Iringa NFRA Frank Felix amesema mpaka sasa kanda hiyo yenye mikoa miwili ina uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 22 na kuongeza kuwa ukasanyaji nafaka utaongezeka mara baada ya maghala mawili yanayo suasua kujengwa yakikamilika.
“Tumepangiwa jumla ya kununua tani elfu 30,ndani ya tani hizo tani elfu tano tutanunua mpunga na elfu 25 tutanunua mahindi,lakini maghala haya mawili yatakuwa na uwezo wa kuchukuwa tani elfu kumi kumi kwa hiyo jumla sasa ya mradi huu ni tani elfu 40”alisema Frank Felix
Akizungumzia changamoto za mradi wa ujenzi wa maghala mawili ya kuhifadhi  nafaka mhandisi mkazi wa TBA Eng.Pedon Mushobozi anasema uzembae wa mkandarasi,hali ya hewa pamoja na kusuasua kwa malipo,yamepelekea kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.
“Changamoto kubwa hapa  ni malipo kwa mkandarasi  na imepelekea mkandarasi kuishiwa fedha”alisema Eng.Pedon Mushobozi
Katika hatua nyingine katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya amewataka wafanya kazi wote wanao fanya kazi chini ya wizara yake kujiendeleza kielimu kwani kufanya hivyo kunaongeza ufanisi kazini.

 Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya akikaua maghala pamoja na kuzungumza na watumishi katika wizara hiyo mara baada ya kufika eneo la ujenzi wa maghala hayo kanda ya Makambako.

 Maghala yanayojengwa katika kanda hiyo ya Makambako mkoani Njombe.
 Baadhi ya nafaka zilizohifadhiwa katika maghala hayo ya kanda ya Makambako.
 Kaimu meneja wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula mkoa wa Njombe na Iringa NFRA Frank Felix akitoa taarifa ya ujenzi wa maghala
 Eng.Pedon Mushobozi akitoa taarifa ya ujenzi mbele ya katibu mkuu wizara ya kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...