Na, Woinde Shizza michuzi Tv, ARUSHA
WAHITIMU wa kidato cha sita mwaka huu wenye ndoto za kusoma Elimu ya juu Nje ya Nchi, wamepata auhueni kwa kupatiwa mkopo wa Elimu ya Juu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Meneja Mkuu wa kampuni ya Global Education Link(GEL) Regina Lema, alisema kumekua na changamoto ya kifedha kwa wanafunzi wanaosoma nje ya Nchi hivyo wao wameamua kuitatu.

Aidha alibainisha kuwa, GEL, kama mawakala wa Vyuo vikuu nje ya nchi, wameamua kutoa Mikopo hiyo ya Elimu ya juu kwa kushirikiana na Mwalimu Commercial Bank pamoja na Amana Bank, ili kusaidia wepesi wa wanafunzi kusoma bila wasiwasi wawapo nje ya Nchi.

"Tumeshuhudia serikali ikiwapa mkopo wanafunzi wa hapa nyumbani(Tanzania) mkopo wa Elimu ya juu kila mwaka, Tumekaa tukawaza, hawa wengine wanaosoma nje ya Nchi wao aanasaidikaje, Sasa tumeona ni bora nao tuwakumbuke, na sisi kama taasisi ya uwakala wa wanafunzi nje ya Nchi, kwakushirikiana na MCB, Na Amana Bank tuwape wanafunzi Wetu mkopo huu ambao utafanyiwa mchakato ndani ya saa 48 Tu" Alisema Regina

Hata hivyo alisema kua kwa sasa taasisi ya GEL ina matawi katika Kanda zote Tanzania, Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya Na Zanzibar, hivyo huduma hiyo itawafikia vijana wote, waliomaliza kidato cha sita ama diploma na wana ndoto za kusoma ama kujiendeleza katika Elimu ya juu nje ya nchi kwa urahisi.

Global education link ni wakala wa Vyuo vikuu nje ya Nchi, anaetambulika na Tume ya Vyuo vikuu Nchini (TCU)ambao wanahusika kuwaunganisha wanafunzi na vyuo vikuu zaidi ya 200 Duniani kwa ajili ya Elimu ya juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...