Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.John Magufuli amewashukuru viongozi wa ngazi mbalimbali kwa kufanikisha kupata wadhamini zaidi ya milioni 1.1 ambao wamemdhamini kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuna kila sababu ya uchaguzi huo kushinda kwa kishindo katika ngazi zote za urais, ubunge, uwakilishi, udiwani na viti maalum.

Akizungmza leo Mjini Dodoma baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi , Dkt.Magufuli amesema kuwa hakutegemea kama angepata wadhamini wengi na anafahamu wenyeviti wenzake wa mikoa wa CCM walisumbuliwa sana kutokana na idadi kubwa ya wadhamini waliojitokeza wakati karatasi zilikuwa chache.

"Mzee Shein(Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein)wewe mwenyewe ulitembeza karatasi ukanipatia wadhamini 800,000 , Umoja wa vijana, UWT,Umoja wa Wazazi na viongozi wote wakiwemo wenyeviti wa mikoa ahsanteni sana .Ahsanteni sana kwa upendo mkubwa mlionionesha, mimi ninajiona nina deni kubwa ambalo ninatakiwa kulilipa kwa kufanya kazi, tumeingia kwenye hatua nyingine ya kwenda kuelezea Ilani yetu ya CCM na kwa namna gani tutawatumikia watanzania.

"Niwaombe viongozi wenzangu wa Halmashauri Kuu pamoja na viongozi wote mpaka kwenye mashina, mabalozi na wananchi wa kawaida tusimame pamoja, tukasimame pamoja ili tuhakikishe ushindi unapatikana.
 
Huwa kuna tabia ya saa zingine kujiamini tumeshashinda, kujiamini ni kubaya mkijiamini saa zingine hamtakwenda kupiga kura na baadae mtajikuta majuto yanakuwa mjukuu, hakikisheni hamuachii nafasi.

"Muende mkahamasishane kwa ajili ya kwenda kupiga kura siku itakapofika , tukachague viongozi wetu ili Chama Cha Mapinduzi kikashinde kwa kishindo, kule Zanzibar tukashinde kwa kishindo kwa kupata wawakilishi wa kutosha , na huku Bara tukashinde kwa kishindo katika nafasi zote za Urais, Wabunge , Wawakilishi,Madiwani na Viti Maalum.Ukawe ushindi mtakatifu na mimi ninaamini katika kazi kubwa zilizofanywa na Serikali zote mbili, katika kazi zote zilizofanywa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa hakuna kitakachotushinda.

"Tufanaikiwa, kwangu mimi nawaona ninyi wajumbe ndio wafalme wa kweli wa kuongoza Taifa hili kwa misingi iliyoimara ya Chama chetu , tembeeni kifua mbele kwasababu mafanikio haya yote ninyi ndio mmeyawawezesha, tunaingia awamu ya pili ya uchumi ni ninyi ndio mmesababisha kwani ndio wasimamizi wa utekelezaji wa Ilani zote mbili za uchaguzi za CCM, ni ninyi ndio mmezuia Corona isisambae kutokana na kushiriki vema kwenye kumuomba Mungu, ninyi ndio ushindi, mnasherehekea ushindi wenu na ushindi huu lazima tuuendeleze,"amesema Dk.Magufuli.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.John Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...