*Azungumzia uhusiano wa Membe kimataifa, asema wamelamba turufu,hawataicha


Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

MWENYEKITI wa ACT Wazalendo Taifa ambaye pia ni Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu Maalim Seif Sharif Hamad amesema kumpata aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe haikuwa kazi rahisi na sasa baada ya kujiunga na Chama kuna watu hawatapa usingizi.

Akizungumza leo Julai 16,2020 wakati wa kumpokea Membe ambaye amejiunga na Chama hicho, Maalim Seif amesema haikuwa kazi nyepesi kumpata Membe kwani vyama vingine mbalimbali vilimtaka lakini ameamua kujiunga ACT Wazalendo.

"Membe mwenyewe amesema yupo nyumbani na hivyo haendi kwingine, namshukuru Membe na mkewe,haikuwa na uamuzi mwepesi. Membe ni turufu, mimi nidhani sio tu kwenda Magogoni,hata Dodoma leo hawalali.

"Membe nafahamiana naye siku nyingi na nilimfahamu zaidi mimi nikiwa Waziri Kiongozi Zanzibar.Membe ni kiongozi jasiri,huwa anasimamia kwenye maamuzi yake,hayumbishwi na mtu.Ndugu wana ACT  niwaambie tumevuna na Chama kitapaa.

"Wakati sisi tunaingia tulikuwa na kauli mbiu ya shusha tanga pandisha tanga na Membe amekuja na awamu ya pili shusha Tanga pandisha Tanga safari inaendelea. Tumeokota na tujifunze kutunza tulichookota,"amesema Maalim Seif.

Amefafanua kwamba Membe amekuwa Waziri wa Mambo ya nje,hivyo anajua na watu wengi,Dunia inamtambua, ana mahusiano mazuri na viongozi wa nchi mbalimbali duniani."Membe anaogopwa na hiyo inatokana na umaarufu wake katika medani za kimataifa.

"Ujumbe wa wanachama wenzangu wa ACT Wazalendo wanakuomba ndugu Membe uchukue fomu ya kugombea urais.Wanachama mnamtaka Membe achukue fomu ya kugombea urais? Kwa jinsi ninavyomjua kwa uungwana wake hatakataa.

"Tumewapokea kwa mikono miwili,kwenye shida na raha,"amesema Maalim Seif ambapo wana ACT waliokuwepo ukumbini kwa kauli moja wamesema wanataka Membe achukue fomu ya urais.

Kuhusu yeye visiwani Zanzibar ambako atagombea urais,amesema kwamba mwaka huu Mungu akipenda atakuwa Rais wa Zanzibar na shikamoo dhidi yake zitatolewa tu."Watu wanaogopa kumpa Maalim Seif shikamoo, mwaka huu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu shikamoo wataitoa,"amesema Maalim Seif.
 MWENYEKITI wa ACT Wazalendo Taifa ambaye pia ni Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza kwenye mkutano maalu wa Kumpokea Mhe.Benard Membe aliyejiunga na chama hicho leo,jijini Dar.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...