Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya wanachama wapya 1,500 wamejiunga na huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maonesho ya Sabasaba yaliyoanza tangu Julai 1, mwaka huu.

Wanachama hao wamejiunga kupitia utaratibu wa Vifurushi vipya ambavyo ni vya Najali, Wekeza na Timiza pamoja na mpango wa watoto chini ya umri wa miaka 18. 

Mbali na wanachama hao wapya, zaidi ya wananchi 2,500 wameelimishwa juu ya umuhimu wa huduma za bima ya afya  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kwamba, kitendo cha Mfuko kuweka na kuwezesha wananchi wote kuchagua huduma wanazotaka kujiunga nazo kumesaidia kwa kiwango kikubwa kurahisisha utaratibu wa kujiunga.

“Tunashukuru Mfuko kwa kushiriki maonesho haya na kutoa huduma za usajili ambazo zimeturahisishia sisi kufika hapa na kujiunga moja kwa moja, huduma za matibabu ni za msingi ambazo zinaleta ujasiri mkubwa ndani ya familia,” Walisema wananchi.

Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa za maonesho na mikusanyiko mingine kwa ajili ya kupata huduma za Bima ya Afya ili kujihakikishia huduma za matibabu.

“Nimefarijika sana hapa kuona wananchi wameamua kujiunga na huduma zetu na kujihakikishia huduma za matibabu na kwa sasa hakuna tena sababu za kushindwa kujiunga kama ilivyokuwa awali, tumeweka utaratibu rahisi sana wa kujiunga unaomwezesha kila mmoja kujiunga na kupata huduma,” alisema Konga.

Alisema kuwa Mfuko umejipanga kupitia ofisi zake zote zilizoko mikoa yote Tanzania kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwafikia katika maeneo yao kuwapa elimu na kuwahamasisha ili wajiunge na huduma.

“Niwahakikishie tu wananchi kuwa Mfuko umejipanga sana kuhakikisha unatoa huduma bora na za haraka kwa wanachama wake na katika kipindi hiki ambacho nchi yetu imeingia kwenye Uchumi wa Kati ni vyema kila mwananchi akawa na uhakika wa kupata huduma za matibabu ili tuweze kuzalisha na kuongeza vipato vya kaya na Taifa kwa ujumla,” alisema  Konga.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga alipotembelea banda la NHIF na kujionea huduma zilizotolewa katika maonesho ya sabasaba

Picha mbalimbali za  utoaji huduma katika banda la NHIF katika maonesho ya Sabasaba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...