Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  Bw. Charles Kichere, akioneshwa kitabu cha bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 toleo la wananchi, na Afisa wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Juma Mfaume wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo Wizara ya Fedha na Mipango  na Taasisi zake inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kuwafikia wananchi na kutoa elimu na huduma mbalimbali.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Msafiri Mbibo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Juma Mfaume, alipokuwa akitoa elimu kuhusu bajeti ya Serikali na namna Serikali inavyosimamia mchakato wa uandaaji na utekelezaji wa bajeti. Katikati ni Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo Bw. Richard Kayombo.
Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Joseph Msumule alipokuwa akieleza Sera, Sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha zenye lengo la kuweka mazingira wezeshi ili kurahisisha usimamizi wa huduma ndogo za fedha katika sekta ya fedha, kutoa elimu kuhimiza watoa huduma ndogo za fedha waweze kujisajili na kupata leseni, katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) wenye lengo la kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma, katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kagaigai, akisaini daftari la wageni alipotembelea  banda la maonesho la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa wa Wizara hiyo Bi. Josephine Majura.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Msafiri Mbibo akimsikiliza Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano kwa Umma wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bi. Shamim Mdee, alipokuwa akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Bodi hiyo, wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake  katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw.  Charles Kichere, akimsikiliza Mchambuzi wa Mifumo wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bi Siganike Baruti, alipokuwa akitoa elimu kwa umma wakati wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...