BODI ya Baraza la Veterinari Nchini imetakiwa kwachukulia hatua watendaji na wataalamu wa sekta ya mifugo wanaofanya hujuma kwa kukamata ng’ombe bila kuwapatia huduma muhimu ikiwemo maji na malisho hali iliyosababisha mifugo mingi kufa huku mingine ikiuzwa kiholela na kusababisha hasara kwa wafugaji.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina leo jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo , Bodi ya Hifadhi ya Bahari, Maeneo Tengefu na Bodi ya Baraza la Veterinali.

Hata hivyo Mhe. Mpina amezuia vishoka wanaotoa huduma za afya kwa mifugo ambapo amesema kuwa hatua za kisheria zichukliwekwa watako bainika kufanya hivyo.

Aidha Mpina ameitaka bodi ya RITA kuanda na kuanza kutekeleza mpango mkakati wa kuanza kutoa mafunzo ya ufugaji kwa wafugaji ili kuongeza wafugaji watakao ongeza uzalishaji.

Lakini pia ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inafatilia kwa ukaribu wahitimu wa ufugaji katika vyuo vya ufugaji kujua wanapomaliza wanakwenda wapi na huko mtaani wanafanya nini.
“ lengo kubwa nikutaka wahitimu hao kuwasaidia wafugaji wenye tija ili kukuzaa ufugaji na kuinua uchumi katika sekta ya ufugaji “ameeleza Mpina.

Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt.Bedan Masuruli,amesema kuwa  Baraza limefanikiwa kufanya ukaguzi wa vyuo sita vinavyotarajia kutoa mafunzo ya ufuganji nchini na huku vyuo vinne vikipewa hidhabati ya kufundisha mafunzo hayo.

Aidha Dkt.Masuruli amesema kuwa kufuta vituo vilivyokiuka maadili ya fugaji hivyo kufungiwa na kutotoa mafunzo hayo na kuwataka kufuata sheria na taratibu juu ya ufugaji ili kuleta ufugaji wenye tija kwa jamii ya watanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...