Mtangazaji na Mwandishi wa Habari nguli nchini Ndugu Jacob Tesha leo ametinga Ofisi za CCM Wilaya ya Moshi kuchukua fomu za kuwania ubunge Jimbo la Moshi mjini. Mgombea amewahi kuwa mtangazaji wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) kwa miaka mingi ambapo alijizolea umaarufu mwingi katika staili yake ya utangazaji na usomaji wa habari kwa Kiswahili na Kiingereza. 
 
Alibuni na kuandaa vipindi vingi vilivyowavutia sana wazee kwa vijana. Baadaye aliteuliwa na Rais kuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu (Press Secretary). Mgombea huyu ana shahada mbili ambazo ni BA (Public Administration and International Relations kutoka Chuo Kikuu cha D'Salaam na shahada ya Uzamili (MA) katika Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) ya Chuo Kikuu cha mt. Augustine. Pia amepata mafunzo…

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...