Katibu wa CCM, Wilaya ya Ilala, Iddi Mkowa akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Ukonga,  Mkuu wa Idara ya Habari na siasa wa vyombo vya habari vya CCM na mjumbe wa NEC, Angela Akilimali leo Jijini Dar es Salam.
 Katibu wa CCM, Wilaya ya Ilala, Iddi Mkowa akimkabidhiwa fedha ya kuchukulia fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Ukonga,  Mkuu wa Idara ya Habari na siasa wa vyombo vya habari vya CCM na mjumbe wa NEC, Angela Akilimali leo Jijini Dar es Salam.
Mkuu wa Idara ya Habari na siasa wa vyombo vya habari vya CCM na mjumbe wa NEC, Angela Akilimali akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MKUU wa Idara ya Habari ya Vyombo vya Habari wa Chama cha Mapinduzi  (CCM)  Angela Akilimali  amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Ukonga.

Akizungumza na waandishi habari mara baada ya kuchukua fomu Angela amesema amefikia uamuzi huo kutokana na katiba ya chama inamruhusu na  kuweza kuwatumikia wananchi atapopitishwa na chama hicho.

Amesema kihistoria yeye ni mwanachama wa muda mrefu na ametumikia wananchi katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama.

Amesema moyo wa kujituma katika chama anao hivyo atapoteuliwa  atakwenda kuwatumikia wanaukonga katika maendeleo.

Amesema kuwa anachosubiri sasa ni  mchakato ndani ya chama akipita hapo ni kuipeperusha bendera ya chama hicho.

Amesema uwezo anao wa kupeperusha bendera hiyo kutokana na kuwa karibu na wananchi wa Jimbo hilo.

Aidha, amesema kuwa kazi ni kuendeleza mazuri zaidi kutokana na sera za Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya kuwainua wanyonge.

Angela amesema Ukonga  akipita ataenda kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi
"Nikiteuliwa ndaani ya chama wanachama wa jimbo kunichagua kwa lengo moja ya kupigania maendeleo ya wana Ukonga na kauli mbiu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kwenda kisasa zaidi  kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa kasi"amesema Angela.

Hata hivyo, amesema kama kijana amekuwa na maono mengi ya kutaka vijana kuinuka kiuchumi katika kuwaunganisha kwenye fursa wanaukonga.

"Nikiteuliwa ndani ya Chama  wanachama wa jimbo kunichagua kwa lengo moja ya kupigania maendeleo ya wana Ukonga na kauli mbiu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kwenda kisasa zaidi  kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa kasi, “ amesema Angela.

Hata hivyo, amesema kama kijana amekuwa na maono mengi ya kutaka vijana kuinuka kiuchumi katika kuwaunganisha kwenye fursa wanaukonga. 

Angellah ambaye pia mwandishi wa habari mkongwe amechukua fomu Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala leo Jumatano tarehe 15 Julai 2020 ni mjumbe wa NEC Taifa. Ameahidi kuwa Kaimu Mkurugenzi wa radio Uhuru.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu na Iddi Mkowa, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Iddi Mkowa amesema Wilaya hiyo ina majimbo matatu ambapo hadi kufikia leo Jumatano saa 6 mchana, Ukonga wamejitokeza 85, Ilala 12 na Segerea 51.

Mkowa amewaomba wanachama  wenye sifa za kuwania uongozi, waendelee kujitokeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...