Bi. Margaret
Karume mwenye uzoefu wa miaka 27 kwenye sekta ya benki
NIC Bank Tanzania Ltd na CBA
Bank Tanzania Ltd wapo mbioni kumalizia uunganaji wa taasisi zao na kuanza kutoa
huduma zao kama NCBA Bank Tanzania Ltd. Wajumbe wa bodi teule wamemteua Bi.
Margaret Karume atakaekua Mkurugenzi na Afisa Mkuu Mtendaji wa NCBA Bank (T)
kuanzia tarehe 8 Julai benki itakapoanza kutoa huduma zake rasmi.
Kwa
sasa Bi. Karume ni Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank Tanzania mwenye uzoefu wa miaka 27
katika sekta ya benki.
‘Huu
ni ukurasa mpya kwa benki hizi mbili. Natazamia kufanya kazi na timu ya watu
wenye nia moja ili kuimarisha taasisi yetu ya fedha nchini Tanzania. Taasisi
hii mpya itaakisi dhamira na maadili kutoka benki zote mbili, baada ya
kujifunza ubora wa pande zote na kujenga taasisi kubwa na bora ya kuwahudumia
wateja na wadau wetu,’’ alinukuliwa Bi. Karume.
Katika
vipindi tofauti, Bi. Karume amewahi kushikilia nyazfa mbalimbali katika sekta
ya benki na kuwa kiongozi wa kuigwa katika ngazi zote za chini hadi juu za
benki. Alipokuwa NIC Bank Group nchini Kenya amefanya kazi kama Mkurugenzi
Mtendaji wa Mikopo Hatarishi. Bi. Karume ana uzoefu imara na taaluma kwenye
maendeleo ya fedha na biashara. Vilevile, ana utajiri na uzoefu katika kuhudumia
wateja wakubwa wa kibenki uzoefu alioupata alipokuwa NIC Group plc na Barclays
Bank Kenya (kwa sasa ABSA Bank).
Anashikilia
shahada ya uzamili katika uratibu duniani (MBA ya Global Executive) na Shahada
ya Sayansi (BSc). Alihitimu elimu ya utawala wa ngazi ya kibiashara kimataifa
kutoka United States International University (USIU) – Africa na stashahada ya
usimamizi wa mahusiano ya wateja kutoka Taasisi ya Kifedha (Uingereza). Vilevile,
yeye ni mwanachama wa Taasisi ya Masuala ya Kifedha, Kenya.
Akithibitisha
uteuzi wake, mwenyekiti mteule wa bodi ya NCBA Bw. Sharmapal Aggarwal
alimpongeza Bi. Karume kwa kuteuliwa kwake.
‘Tunatambua
uzoefu wake mkubwa kwenye sekta ya benki na tunasifu kwa kujitoa kwake upya
kwenye benki. Tunaamini kuwa yeye ni mtu sahihi kuiongoza Benki ya NCBA kwenye zama
mpya ya maendeleo endelevu na kuleta mafanikio kwa wadau wote Tanzania na bara
la Afrika kwa ujumla,’’ alinukuliwa. Vilevile alibainisha kuwa Bw. Gift Shoko
ambaye ni Afisa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CBA Tanzania ni mteule katika bodi
ya benki ya NCBA kama Mtendaji Mkuu, na ameteuliwa kuiongoza taasisi mpya kama
Mkurugenzi Mtendaji wa biashara za kidijitali na wateja wadogo na wakubwa
Nafasi
yake itaiongoza benki ya NCBA kwenye biashara za kidijitali ambapo ni kiini cha
ukuaji endelevu wa biashara ya kundi hili wakati inalenga kuwa benki
inayoongoza kwenye kanda katika miaka mitano ijayo.
"Kuleta
benki zote mbili pamoja imetuwezesha kukua na kuwa benki kubwa katika sekta ya
digitali. Kadri ambavyo teknolojia inaendelea kukua tunashuhudia teknolojia
ikiwa inachukua nafasi muhimu zaidi katika kuleta ushirikishwaji wa kifedha
nchini Tanzania, Afrika Mashariki na kwa bara zima kwa ujumla. Tuna vifaa, rasilimali na wataalamu wa
kutuwezesha kuongoza katika soko, "Alisema Bwana Shoko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...