Said Mwishehe, Michuzi TV.

HATIME Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Rais Dk.John Magufuli amefichua siri kuhusu aliyekuwa amependekeza awe mgombea mwenza wake(Makamu wa Rais) wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kwamba alikuwa anataka awe Dk.Hussein Mwinyi au Mama Samia Suluhu Hassan.

Dk.Magufuli amefichua siri hiyo leo Mjini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu ambao pamoja na mambo mengine umepitisha jina lake kwa kishindo kugombea tena urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. "Sijawahi kusema kokote lakini leo hii naomba nitoe hii siri nilipokuwa nimechaguliwa kwa mara ya kwanza niliowachagua kuwa wagombea mwenza, nilimchagua Mama Samia na Dk.Hussein Mwinyi. Ukweli ni kwamba ukishindanishwa na mwana mama utashindwa tu, wanatushinda kwa mambo mengi.

"Mzee Jakaya Kikwete na Mzee Mkapa wako hapa ni mashahidi, hivyo katika nafasi hiyo akashinda Mama Samia na hakika amekuwa akifanya kazi nzuri sana huyu mama.Hivyo kwa wakati ule nikamwambia Dk.Hussein Mwinyi ngoja niende na Mama,ni mama safi sana, ndio maana nilipotaja jina la Mama alianza kulia kwani hakuwa akitarajia.

"Dk.Hussein Mwinyi alikaa kimya,hakuwahi kulalamika, hivyo baada ya kuingia madarakani nikamchagua kuwa Waziri wa Ulinzi, unapochagua Waziri wa Ulinzi lazima awe mtu unayemuamiani sana maana majeshi yote ya ulinzi na usalama yanakuwa chini yake,"amesema Rais Magufuli mbele ya wajumbe hao.

Akimzungumzia zaidi Dk.Hussein Mwinyi, Rais Magufuli amesema anatosha sana kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibara na atashanfaa iwapo kuna watu watasema Mwinyi hatoshi.Kuhusu Dk.Hussein kuwa mpole, Dk.Magufuli amesema sio mpole bali ni mnyenyekevu sana, anajua kutunza moyo wake."Kama atachaguliwa Mwinyi...kama atachaguliwa mtayaona matokeo.Nawashauri ndugu zangu achaneni na Upemba, achaneni na Uunguja, achaneni na Ukaskazini.

"Mimi nimemzidi Dk.Hussein Mwinyi,amezaliwa katika kipindi cha Mapinduzi matukufu.Nitashangaa kuwa na Rais wa Zanzibar ambaye nitakuwa namuamkia,Shikamoo.Msinichagulie shikamoo huko Zanzibar nitapata shida ndugu zangu,nataka nikija Zanzibar niwe nafuraha zote.

"Mkimchagua Dk.Hussein Mwinyi Zanzibar itapaa,mkimchagua Mwinyi nitamsaidia kwa nguvu zangu zote maana ni mdogo wangu,"amesem Dk.Magufuli na kuongeza kuna watu ambao wanasema kuna usultani, lakini kwa Dk.Hussein ndio kwanza anagombea sasa huo usultani unatoka wapi? "Wapo masultani ambao wamekuwa wakigombea kila uchaguzi mkuu na wanashindwa lakini bado wapo tu".

Ametumia nafasi hiyo kushauri vyama vya siasa viwe na utaratibu wa kuweka watu tofauti tofauti na sio mtu mmoja kila wakati wa uchaguzi."Tuwe na utamaduni wa kukubali kumpumzika sio lazima uwe wewe tu. Kwa hiyo nawapongeza viongozi wa vyama vya siasa ambao wanaachia wengine.Napenda kuwahakikishia mimi na Mwinyi tutashirikiana. najua kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu wapinzani hamtashinda lakini kuna mahali tutakwenda pamoja.

"Hata hivyo niwashauri vyama vya siasa sisi sote ni wamoja, tuendelee kushirikiana katika kuijenga nchi yetu.Vyama vingi vinajiendesha kwa utaratibu mzuri sana,ukiondoa vyama vichache.Katika uchaguzi mkuu tunapokuwa majukwaani hatuna sababu ya kutukanana na kuhubiri lugha za kutengenanisha watu, na badala yake wanasiasa wahubiri umoja na msikamano".

Wakati huo huo Rais Magufuli amewashukuru marais wastaafu kwa mchango wao wa nyakati tofauti wa kulifikisha Taifa la Tanzania lilipofikia kimaendeleo huku akitumia nafasi hiyo kuwashukuru wasanii kwa mchango mkubwa na amekuwa akipata clips mbalimbali, hivyo ameahidi kuendelea kushirikiana nao na watashiriki kikamilifu kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...