Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii
SHIRIKA la Save The Children leo Julai 9 limekabidhi vifaa maalumu vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona yakiwemo matanki, sabuni za kunawia na taulo za kike kwa Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni huku vifaa hivyo vikielekezwa kuwafikia wanafunzi katika mashule mbalimbali ikiwa ni sehemu mchango wa Shirika hilo kwa Serikali katika kupambana na kuenea kwa virusi vya vya Corona hasa kwa wakati huu ambao shule zimefunguliwa na watoto wanaendelea na masomo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Dkt. Samwel Laizer amesema kuwa Save The Children wamekua wadau na washirika bora katika kulinda na kutetea watoto pamoja na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi.

"Mmekua mkifanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali, ni mfano mzuri wa kuigwa na nina imani vifaa hivi vitawafikia walengwa"ameeleza Laizer.

Dkt.Laizer amesema kuwa baada ya watoto kurejea mashuleni bado wanatakiwa kuwa salama kiafya ili waweze kusoma kwa uhuru na kufaulu masomo yao.

" Mchango huu ni hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto za watoto wetu, wanafunzi watanawa kwa kutumia vifaa hivi na kuingia madarasani wakiwa salama zaidi na kusoma kwa uhuru zaidi" ameeleza.

Akizungumza kwa niaba ya Shirika hilo Meneja wa Uchechemuzi na Kampeni kutoka shirika hilo Nuria Mshare amesema kuwa wamekabidhi matanki 20, sabuni za kunawia 500 pamoja na taulo za kike 1000 kwa Manispaa ya Kinondoni ili ziwafikie na kuwasaidia watoto ambao wamerudi shule.

Amesema kuwa lengo kutoa mchango huo ni kutokana na ufanyaji kazi kwa ukaribu zaidi wa Serikali na shirika hilo katika kuhakikisha mtoto analindwa hasa katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona vilivyoathiri duniani kote.

"Tulivyoona wanafunzi wanarudi shule kuendelea na masomo yao tukaona ni muhimu kuisaidia Serikali katika kuhakikisha watoto wanakua salama kiafya kwa kuhakikisha wananawa na kupata elimu ya afya sambamba na kupata elimu bora zaidi" ameeleza.

Shirika lisilo la kiserikali limekuwa likifanya kazi na shule zipatazo 10 katika Mkoa wa Dar es Salaam na wamekuwa wakishirikiana kwa karibu zaidi na Serikali katika kuhakikisha watoto wanabaki salama pamoja na kupata mahitaji yote ya msingi ikiwemo elimu na afya.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Samwel Laizer (kulia) akipokea vifaa maalumu vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa shule mbalimbali Wilaya humo kutoka kwa Meneja wa Uchechemzi na Kampeni kutoka Save The Children Nuria Mshare (katikati) kushoto ni Meneja wa mradi wa ulinzi kwa mtoto Jesca Ndana, leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona vilivyotolewa na Shirika la Save The Children kwa Manispaa ya Kinondoni vikielekezwa kuwafikia  wanafunzi katika mashule mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kupambana na kujikinga zaidi na kuenea kwa virusi hivyo, leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa mradi wa ulinzi kwa mtoto Jesca  Ndana (wapili kushoto) akitoa maelezo kwa Mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Samwel Laizer juu ya namna wanavyozihudumia shule 10 za Mkoa wa Dar es Salaam katika kuhakikisha mtoto analindwa na kupata mahitaji ya msingi, leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...