Mkurugenzi wa Shirika la Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzani David Mlongo  akiwa kwenye shamba la nyanya la wanawake wajane wilayani Mufindi mkoani Iringa 
Mkurugenzi wa Shirika la Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzani David Mlongo  akiwa kwenye shamba la nyanya la wanawake wajane wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Wanawake wa kikundi cha akina mama Wajane cha kijiji cha Iyela wakiwa kwenye shamba la nyanya 

Fredy Mgunda, Mufindi

USHIRIKIANO baina na Serikali ya Wilaya ya Mufindi na Shirika la kuhudumia watoto SOS unatajwa kuimarsha uchumi wa kundi la wanawake vijijini wakiwemo wajane waliokuwa wakikabiliwa na hali duni ya kipato na kushindwa kuhudumia familia.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi Robert Sungura alisema mradi wa uwezeshaji wanawake kiuchumi umesaidia wanawake walio wengi kujiongezea kipato kwa kuanzisha shughuli za ujasiriamali ikiwemo kilimo biashara


Miongoni mwa wanawake wa kikundi cha
akina mama Wajane cha kijiji cha Iyela wakizungumza wakati wa ukaguzi wa shughuli za maendeleo ya vikundi wameeleza kuwa uwezeshwaji huo umewasaidia kukidhi mahitaji ya familia.


Jumla ya Kaya 250 za wanawake wajane zinazolea watoto wapatao 928 Wilayani Mufindi Mkoani Iringa walisema muda mwingi walikuwa wakitaabika juu ya malezi ya watoto walioachiwa na wenzi wao
waliotangulia mbele za haki.


Wanawake hao walisema kuwa
wamefaidika na mradi uwezaji wanawake kiuchumi unao fadhiliwa na Shirika la Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzania kwa Kilimo cha Nyanya na Mahindi ambacho kimebadilisha maisha ya Akinamama hawa wa Kijiji cha Iyela ambapo kimewafanya waweze kusomesha watoto,kujenga Nyumba na Kuongezeka kwa Mazao kupitia elimu bora ya kilimo cha kisasa.


“Furaha ya wanawake hawa miongoni mwao wakiwemo wajene ni juu ya mafanikio ya kiuchumi waliyoanza kuyapata kutokana na mradi wa uwezeshwaji wanawake unaotekelezwa na shirika la Shirika la kuhudumia watoto SOS kwa ushirikiano na Serikali ya wilaya ya Mufindi”


Wanawake hao waliongeza kuwa hapo awali walikuwa wanapata kiasi cha gunia mbili za mahindi na kuwapelekea kwenda kufanya kibarua sehemu nyingine lakini baada ya elimu iliyotolewa na Shirika la Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzania imewaongezea kipato cha mazao
hadi kufikia kugunia kumi na saba.


 Afisa Miradi wa Shirika hilo anayesimamia Kilimo Doto Solo alisema kuwa wanawake hao wajane walikuwa wamekata tamaa kutokana na ugumu wa maisha wengi wao wakishindwa kuhudumia familia wakiamini kuwa hakuna njia mbadala ya kujikoma kiuchumi hata jitihada za Shirika la SOS kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Mufindi zimefanikiwa kubadilisha mtazamo hasi waliokuwa nao awali na sasa wamekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake wengine.


Wengine walikuwa na changamoto ya chakula kabisa wengine walikuwa wanahangaika kununua na kutafuta msaada kwa wadau wengine hata ukiwaambia habari za vikundi na shughuli za kiuchumi ilikuwa vigumu kuwaeleza ila mara baada ya kutoa elimu sasa wamekuwa mfano kwa wanawake wengine.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika La SOS Tanzania David Mlongo alitoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kuongeza Kiwango cha Mikopo kwa Vikundi vinavyofanya Vizuri katika Uzalishaji  huku akiihimiza Halmashauri kushirikiana zaidi kuwawezesha wanufaika hao kuanzisha kilimo cha kisasa kwa kutumia nyumba kitalu


Mlongo alisema kuwa mikopo hiyo itasaidia wanawake hao kuwekeza kwenye vitalu nyuma  kutokana na mikopo ambayo watakuwa wamekopeshwa kwa kuwa kilimo cha aina hiyo kimekuwa na faida kubwa kuliko kilimo cha kawaida kwa kuwa kilimo hicho hakina changamoto nyingi.


Lakini Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Robert Sungura aliwahimiza wananchi wa wilaya ya Mufindi wakiwemo wa wanawake pamoja na vijana kutokata tamaa katika suala la kujikwamua kiuchumi na badala yake waanzishe vikundi vyenye lengo la kiuchumi na serikali iko tayari kuwawezesha kupitia mikopo yenye masharti nafuu.


Shirika hilo la SOS pia limewawezesha wanawake wa Kikundi cha Omaji kijiji cha Ukelemi ambao wanajihusisha na Kilimo cha Umwagiliaji ambao kwasasa kipato chao kimepanda kutokana na kuvuna mazao kwa wingi hususani Mahindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...