Wahumini 500 waliopona Corona kutoka kanisa la Shincheonji tawi la Daegu wamejitolea kuchangia utegili ( blood plasma )
Kwa kipindi ambacho mamlaka Zinaharakisha kutafuta tiba ya korona kwa kutumia utegili (blood plasma ) ya watu ambao wameugua virusi vya korona na kupona,waumini wa kanisa la shincheonji Tawi la Daegu wamejitolea kuchangia utegili.
Mamlaka ya kudhibiti na kuzuia magonjwa Korea (KCDC) imesema itaweka magari matano ya kuchabgia damu chuo kikuu cha KYUNGPOOK kwa muda wa siku tano kuanzia leo tarehe 13  mwezi huu wa saba,wakishirikiana na msalaba mwekundu kwa ajili ya upatikanaji wa utegili(plasma) hizo kutoka kwa waumini 500 wa kanisa la Shincheonji ambao wamepona kabisa virusi hivyo vya corona.
Mnamo mwezi wa sita mwaka huu kanisa la Shincheonji lilionesha nia ya kutaka kuchangia utegili(plasma) kutoka kwa waumini 4000, lakini waumini 55 pekee ndio walioweza kuchangia utegili(plasma), mnamo tarehe 10 mwezi wa sita,kwa sababu ya uwezo wa hospitali tatu tu ambazo zilikuwa na uwezo wa kupokea mchango huo wa utegili(plasma).
Kanisa la Shincheonji lilisema kuwa kuna uwezekano wa kupata utegili(plasma) kutoka kwa waumini 500 kwa muda wa wiki moja, kama magari ya kuchangia damu yatatumika ili kuongeza wingi wa uchangiaji huo.
Mpaka sasa watu 170 wameshachangia utegili(plasma) katika Taifa lote,na majaribio ya tiba yanatarajiwa kuanza wiki hii.Utegili(plasma) ambayo itachangiwa na waumini 500 kutoka kanisa la Shincheonji itatumika kutengeneza  dawa baada ya majaribio.
Mhumini mmoja wa kanisa la Shincheonji mji wa Daegu alisema “naomba Mungu damu hii inayochangiwa na waumini itakuwa ni hatua kubwa  katika jitihada za kutokomeza Corona nchini Korea na ulimwenguni kote”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...