ZAIDI ya wanawake 22 wamechukua  fomu  ya kuwania nafasi ya ubunge wa  Viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Ruvuma ikiwa ni idadi kubwa zaidi kwa wanawake kujitokeza kugombea nafasi hiyo katika mkoa huo.


Katibu wa Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Mkoa wa Ruvuma Rukia Mkindu amesema kuwa wakinamama wanaendelea kujitokeza katika uchukuaji wa fomu hizo na kuwa hadi sasa ni zaidi ya 20 wamechukua na wengine wameshazirejesha.

 Mkindu amesema kuwa kabla ya kuwakabidhi fomu hizo wagombea hao wanapewa maelekezo mbalimbali ikiwemo na namna ya ulipiaji wa fomu hizo kuziingiza kwenye akaunti husika na kisha kukabidhiwa fomu na kuzijaza.

 Baadhi ya waliochukua fomu hizo kuwa ni Sabina Mbena Lipukila ambaye amechukua saa 4:26 asubuhi ni mwalimu anatokea Chama Cha Walimu (CWT) na wengine ni Happiness Ngwando ambaye tayari fomu yake ameshairejesha saa 4:38 asubuhi ,mhandisi Anifa Chigumbe ambaye ameschukua saa 4:10.

 Wengine ni Habiba Mfaume Asiya na Upendo Ndunguru  hao ni  sehemu ya baadhi ya waliochukua fomu kuwania nafasi hiyo huku katibu wa Jumuiya hiyo amewataka wachukuaji fomu hao kuzingatia maagizo yaliyowekwa na chama ili yasifanyike makosa katika ujazaji fomu hizo.

Hata hivyo idadi hiyo inaweza kuongezeka kwani muda wa kuchukua fomu bado upo na utamalizika tarehe 17 Mwezi huu na kuwataka wanachama wa jumuiya hiyo kujitokeza kuchukua fomu za kuomba kugombea Ubunge wa viti maalum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...