Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wasaidizi wa kisheria nchini wameelezwa kuzingatia maadili katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wahitaji ili waweze kupata nafuu na haki inayohitajika kwa mujibu wa sheri.

Wito umetolewa na katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome wakati akizindua kamati ya uratibu wa shughuli za msaada wa kisheria mkoa wa Njombe.

“Katika kazi ni wajibu kuhakikisha maadili yanazingatiwa,maadili katika maeneo mbali mbali,maadili katika ushauri,kupeleka kesi mahakamani na maadili katika mahusiano yetu na watu ambao tunawahudumia,na mtoa msaada wa kisheria hawezia akawa mchonganishi”alisema Prof.Sifuni Mchome

Aidha Mchome amesema lengo mojawapo la serikali kuwa na wasaidizi wa msaada wa kisheria ni kusaidia katika utetuzi wa migogoro inayojitokeza katika jamii pamoja na kuhakikisha uwepo wa utawala bora.

Naye mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameiomba wizara ya katiba na sheria kuongeza nguvu katika kuzisimamia asasi zinazotoa elimu kutokana na uwepo wa asasai zinazofanya kazi isiyokuwa na afya kwa taifa.

“Kwa muda mrefu huko nyuma asasi hizi zingine zilikuwa zikifanya kazi ambazo hazina afya kwa ustawi wa nchi na wengine wamekuwa ni madalali wa kusimamia maslai ya nchi zingine za ughaibuni”alisema Ole Sendeka

Kaimu aifisa maendeleo ya jamii mkoa wa Njombe Farahani Kanyenda,amesema wasaidizi na watoa huduma za msaada wa kisheria wamekuwa na msaada mkubwa kwa jamii na kuwezesha idadi ya watu waliopata huduma ya msaada wa kisheria kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Mei 20 kufika 8282 kwa upande wa madai,19 kwa upande wa Jinai,26 kwa upande wa matunzo huku watoto waliopata msaada wa kisheria wakiwa 42.

Erasto Mkiwa ni mratibu wa shirika la PAD na Geofrey Kaduma ni mkurugenzi wa kituo cha msaada wa sheria Njombe,wanasema licha ya uwepo wa changamoto katika shughuli zao lakini wanaamini kamati iliyoundwa itasaidia kuwafikia zaidi wananchi wenye migogoro mbali mbali.

“Kwa kupitia kamati hii itatusaidi kuwafikia zaidi wananchi kwasababu ni sehemu mojawapo ya kurahisisha mawasiliano na kupitia wadau tuliopo ni rahisi kuelewa wapi kuna tatizo”Alisema Erasto Mkiwa.
 Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakati alipofika mkoani Njomba kwa minajili ya akizindua kamati ya uratibu wa shughuli za msaada wa kisheria katika mkoa huo.

 Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome akizungumza na wadau wa sheria pamoja na asasi mbalimbali mkoani Njombe wakati wa kamati ya uratibu wa shughuli za msaada wa kisheria katika mkoa huo.
 Maafisa wa serikali,wadau wa sheria na Asasi mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome mara baada ya uzinduzi wa kamati ya uratibu wa shughuli za msaada wa kisheria mkoa wa Njombe uliofanyika ukumbi wa JD Hotel mjini Njombe.
 Baadhi ya wadau wakiwa makini na kumsikiliza katibu mkuu wa katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome.


  Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome akikagua ujenzi wa jengo la ofisi za mahakama mkoa wa Njombe zinazojengwa eneo la Lunyanywi mjini Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...