Na Shukrani Kawogo, Njombe

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Sunday Deogratius amewataka vijana na wakina mama kujitokeza kufanya vibarua katika miradi mbalimbali inayoendeshwa na halmashauri hiyo ili kuweza kujipatia kipato.

Hayo aliyasema alipokuwa akikagua ujenzi wa shule ya kisasa ya Nicopolis Academy ambayo inaendelea na ujenzi wake ambapo kwa sasa imeshakamilisha jingo la Utawala, madarasa matatu na matundu ya vyoo.

Alisema vijana na wakina mama wanapaswa kuchangamkia fursa za vibarua zilizopo katika miradi mbalimbali ikiwemo miradi inayotolewa na halmashauri hiyo.

“Nimefurahishwa sana kuona wakina mama na vijana mmepata kazi ya kuwa vibarua katika mradi huu wa ujenzi wa shule ya Nicopolis Academy hivyo nawapa hongera sana kwa kuwa wapambanaji”. Alisema Deogratius.

Aidha alisema amekuwa akishirikiana na mmiliki wa shule hiyo Augustino Mwinuka toka hatua za awali kwa kutuma wataalamu wake kwaajili ya kukagua ubora wa majengo hayo.

Alisema ofisi yake inashirikiana na sekta binafsi katika kukuza maendeleo ya jamii hivyo baada ya mmiliki wa shule hiyo kuwashirikisha juu ya ujenzi huo wa shule bora walimpa wataalamu pamoja na ramani ya majengo ya shule hiyo.

“Shule hii ni bora na ya kisasa katika wilaya hii, tuliona ni jambo jema kusaidiana na mmliki wa shule katika kuijenga shule hii kwa kutoa ushauri wa kitaalamu ili iweze kuwa katika muonekano bora zaidi”. Alisema Deogratius.

Sanjari na hayo Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa vijana, wakina mama na wasiojiweza kuunda vikundi na kujitokeza kuchukua mikopo ya serikali isiyo na riba ambayo hutolewa na halmashauri yake.

Alisema mwitikio wa mikopo hiyo umekuwa mdogo na wamejikuta kwa mwaka huu wa serikali wa fedha wakifunga huku wakiwa wamebakiwa na fedha ambazo zilitakiwa ziwe kwa wananchi.

Aidha kwa upande wa mmiliki wa shule hiyo Augustine Mwinuka amesema shule hiyo itawasaidia watoto wasiyo jiweza na waishio katika mazingira magumu lakini pia kwa wale wenye uwezo watakaohitaji watoto wao wasome hapo watalazimika kuchangia gharama kidogo.

Aliongeza kuwa ujenzi huo unatarajia kukamilika mwezi Desemba Mwaka huu na majengo hayo kuanza kutumika mwezi January mwaka ujao ikiwa na vyumba nane vya madarasa, jengo la utawala, jengo la waalimu, mabweni ya wanafunzi pamoja na matundu ya vyoo.

Naye mmoja wa vibarua waliopo katika ujenzi wa shule hiyo Josephina Haule ametoa shukrani kwa niaba ya wenzake na kusema kuwa kufika kwake mkurugenzi huyo katika eneo hilo kumewaongezea uelewa kwa baadhi ya vitu ambavyo walikuwa hawavifahamu.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Ludewa Sunday Deogratius akiwa kwenye picha ya pamoja na mmiliki wa shule ya Nicopolis Academy pamoja na vibarua wa ujenzi wa shule hiyo
 Mmiliki wa shule ya Nicopolis Academy akipewa maelezo na Fundi mkuu wa ujenzi wa shule hiyo Anzawe Mtewele
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Mkoani Njombe, akizungumza na vibrua wanaofanyakazi katika ujenzi wa shule ya Nicopolis
 Mkurugenzi wa Halmashauri Ludewa Mkoani Njombe Sunday Deogratius akikagua jengo la walimu linalojengwa katika shule ya Nicopolis Academy.
Mkurugenzi wa Halmashauri Ludewa Sunday Deogratius ( kushoto) akiwa ameongozana na mmiliki wa shule ya Nicopolis Academy Augustine Mwinuka wakati wakikagua vyumba vya madarasa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...