WATANZANIA 100 walilondoka nchini kinyume cha sheria na kutokomea Afrika Kusini, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuondoka nchini bila kufuata taratibu za uhamiaji.

Watuhumiwa hao, ambao wengi wao wameonekana kuwa ni Vijana wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ambapo wote wamekiri kutenda kosa hilo na wameiomba mahakama iwasamehe.

Hata hivyo, Hakimu Simba amesema kuwa haoni faida yoyote ya kuwapeleka watuhumiwa hao gerezani haswa katika kipindi hiki ambacho kuna gonjwa hatari la Corona.... 


"Sioni faida yoyote ya kuwapeleka gerezani lakini mahakama inawapa onyo kali na inawaachia kwa masharti msirudie kutenda kosa hili kwa miezi sita, amesema Hakimu Simba.

Mapema wakisomewa shtaka lao na wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji GodfreyNgwijo.

Inadaiwa, Julai 3, 2020 huko katika uwanja wa Ndege wa Juliys Nyerere  uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote 100 walikutwa wakiwa wameondoka nchini  kinyume cha sheria bila kufuata utaratibu wa kutoka na kuelekea Afrika Kusini.

Wakisomewa Maelezo ya awali imedaiwa katika tarehe zisizojulikana washtakiwa hao waliondoka nchini bila kufuata utaratibu na kwamba Julai 3 mwaka huu watuhumiwa walirudishwa nchini Tanzania baada ya uchunguzi na kugundulika kuwa ni wahamiaji haramu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...