Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa Uendelezji wa Viwanda Vidogo na vya Kati.Uzinduzi ulifanyika jijini  Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Prof. Joyce Ndalichako, kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa, na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi yake anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji  Bi. Dorothy Mwaluko anayemfuata ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe na wa kwanza kushoto ni Katibu Mktendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’I  Issa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Uendelezji wa Viwanda  Vidogo na vya Kati.Uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.
Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza masuala yanayohusu viwanda na biashara wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Uendelezji wa Viwanda Vidogo na vya Kati ulifanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Profesa Joyce Ndalichako,akieleza fursa katika sekta ya elimu kwa washiriki wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Bw.William Erio akielezea jinsi walivyosaidia wajasiliamali wakati wa  uzinduzi wa Mpango wa Uendelezji wa Viwanda  Vidogo na vya Kati.Uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Prof.Silvester Mpanduji  uzinduzi wa Mpango wa Uendelezji wa Viwanda  Vidogo na vya Kati.Uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’I Issa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Uendelezji wa Viwanda  Vidogo na vya Kati.Uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki katika hafla ya Uzinduzi wa Mpango wa Uendelezji wa Viwanda  Vidogo na vya Kati uliofanyika Julai 10, 2020 Ukumbi wa Hazina Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa wakicheza na kufurahia wimbo maalum wa kuipingeza Serikali katika mapinduzi ya viwanda ulioimbwa na Msaanii Bw. Mrisho Mpoto wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Profesa Joyce Ndalichako (kuli kwake)  na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (kushoto kwake) pamoja na viongozi walioshiriki katika uzinduzi wa Mpango wa Uedeshaji wa Viwanda Vidogo na vya KatiJijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa wakimsikiliza Mama Kaminyoge akitoa maelezo kuhusu vyakula vya kusindikwa vya aina mbalimbali wakati wa maonesho ya wajasiriamali walioshiriki katika uzinduzi huo Jijini Dodoma
…………………………………………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua Mpango wa Uendelezaji wa Viwanda Vidogo na vya Kati wenye lengo la kutatua changamoto ya upatikanaji wa ujuzi, masoko na mitaji katika miradi midogo na vya kati (SMEs) nchini.
Uzinduzi huo ulifanyika mapema Julai 10, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage Hazina Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe.
Pia ulihudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za SIDO, VETA, NEEC, NSSF na Banki ya AZANIA pamoja na Viongozi na Wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali za Sekta binafsi, Wajasiriamali na Wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mhagama amesema uwepo wa mpango huo utasaidia kuongeza kasi ya ujenzi na ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira wezeshi na kuandaa mazingira yenye mfumo wa kibiashara yatakayorahisisha kutengeneza uzalishaji wenye tija na kuunda soko la bidhaa utakaoboresha na kuinua maisha ya Watanzania.
“Serikali imetengeneza fursa za kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kujipatia kipato na kuhakikisha inatatua changamoto mbalimbali zinazokabili nguvu kazi ya taifa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu na ujuzi wa kutosha pamoja na ukosefu wa mitaji na masoko ya uhakika wa bidhaa zinazozalishwa”,alisema Waziri Mhagama.
Waziri alifafanua kuwa mpango umejikita katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanasaidiwa kuongeza ujuzi, kupata uzoefu na kuwawezesha kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na nje. Aidha, Mpango huu pia unalenga kuwezesha viwanda kupata vifaa vya kisasa  kama mitambo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji ili uwe na tija, kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kupanua shughuli za uzalishaji pamoja na kuongeza kinga za  hifadhi za jamii kwa wajasiriamali.
“Kupitia mpango huu wenye viwanda na wajasiriamali wamepanuliwa fursa ya kupata mitaji hivyo kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi wanaohitimu vyuo katika ngazi mbalimbali,”Alisistiza Waziri
Aliongezea kuwa, Mfumo unajikita kuwafika wananchi wote bila ubaguzi na matabaka ya aina yoyote kwa kuzingatia vigezo na masharti nafuu yaliyopo katika mfumo huu.
“Programu hii inavunja matabaka baina ya makundi mbalimbali katika jamii na kutoa fursa sawa kuanzia mtu binafsi hadi vikundi katika kuwapatia mitaji na ujuzi sawa hivyo tuiunge mkono kwani inawalenga Watanzania wote,” alisema
Aidha alibainisha sekta ya viwanda imeendelea kuwa na tija katika kuchangia ongezeko la Pato la Taifa kwa kuongezeka kwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ambapo Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2019 ilikuwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 8.05 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 0.45 na hii ni matokeo ya kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji viwandani katika kipindi hicho pamoja na kasi ya ukuaji wa thamani ya Uzalishaji Bidhaa Viwandani kwa mwaka 2019 ambayo ilikuwa ni Shilingi Trilioni 10.2 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 9.6 mwaka 2018, sawa na kasi ya ukuaji wa asilimia 5.8
Waziri aliendelea kutoa wito kwa taasisi husika kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu fursa zilizopatikana katika program na kuvitumia vyombo vya habari katika kueleimisha umma kwa malengo ya kuwafikiwa wengi pamoja na kuzitaka taasisi za kibenki kutoa mikopo kwa wajasiriamali kwa mifumo rafiki na inayofikika pamoja na kuutaka uongozo wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuwa na program za tathimin utekelezaji wa mpango kwa vipindi mbalimbali.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alieleza furaha yake ya uwepo wa mpango huo kwani umesadifu mikakakti ya nchi katika uendelezaji viwanda na kusema imekuja wakati mwafaka kwa kuzingatia imelenga sekta zenye tija katika kutoa ajira kwa watanzania wengi kwani imefungamanisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuwa ndizo zenye mchango mkubwa katika ajira.
“Ni hakika kuwa, kupitia Mpango huu wa uendelezaji wa viwanda, ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika  mnyororo mzima wa thamani wa sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji zitaongezeka na kupunguza changamoto mbalimbali zinazokabili jamii kutokana na ongezeko la wasio na ajira nchini,”Alisema waziri Bashungwa.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’I Issa alisema, mpango umeainisha namna bora ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo la kukuza mitaji na kuimarisha vyanzo vyao vya mapato na kukuza akiba na mikopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...