WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameipongeza Wakala ya Bishara na Leseni (BRELA) kwa kuboresha huduma zake.

Haya yamejiri leo Julai 3, 2020 alipotembelea banda la BRELA la maonesho ya Sabasaba kwenye Viwanja vya maonesho vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupata maelezo kuhusu lengo kuu la BRELA kushiriki maonesho ya 44 ya Sabasaba pamoja na hatua kubwa iliyopigwa katika utoaji wa huduma kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu BRELA, Godfrey Nyaisa, alibainisha wazi kwamba amefurahishwa na huduma ya utoaji wa huduma papo kwa hapo.

“Sikutarajia kushuhudia mteja akifanya usajili na kupata cheti chake hapa hapa, hakika hii ni hatua kubwa mmefikia katika kuhakikisha kwamba mnatengeneza mazingira mazuri kwa Wafanyabiashara hapa nchini ili waweze kurasimisha biashara zao.” Alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha akizungumza katika hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa maonesho ya 44 ya Sabasaba, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameitaka BRELA pamoja na taasisi zingine zilizo chini ya Wizara yake kuboresha mikakati yake ya kuwafikia Wananchi katika Halmashauri zao.

Ameeleza kwamna pamoja na kuboresha huduma zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara sasa ni wakati wa kuwafikia wananchi katika Halmashauri zao na kuwapatia huduma kwa haraka, hivyo ni muhimu kwa BRELA pamoja na Taasisi zilizo chini ya Viwanda na Biashara kuhakikisha zinaboresha mikakati yao ya kutoa huduma katika maeneo hayo.

Awali akizungumza na vyombo vya Habari katika banda la BRELA la maonesho ya Sabasaba, Afisa Mtendaji Mkuu BRELA, Godfrey Nyaisa alibainisha kwamba lengo kuu la kushiriki katika maonesho hayo ni kuhakikisha kwamba Wananchi wanapata huduma na utatuzi wa changamoto zao zote papo kwa papo.

“Tunataka Wananchi watambue kwamba BRELA ya sasa sio kama ile ya zamani, mambo yamebadilika. Tupo hapa leo kudhihirisha hilo kwa utoaji wa huduma za papo kwa hapo.

Pamoja na mambo yote tupo hapa pia kujibu hoja za Wananchi ana kwa ana, kutoa elimu kuhusu huduma tunazotoa na kuelezea kwa namna gani hivi sasa BRELA tumeboresha mifumo yetu.”

Ni wito wangu kwa kila Mwananchi anayehitaji huduma za BRELA kufika katika banda letu lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ili kuweza kupata huduma yeyote anayohitaji hapo hapo.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa (kushoto) akilezea lengo kuu la BRELA kushiriki maonesho ya 44 ya Sabasaba pamoja na hatua kubwa iliyopigwa katika utoaji wa huduma alipotembelea katika banda la BRELA la maonesho ya Sabasaba kwenye Viwanja vya maonesho vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2020. Katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) akimkabidhi cheti cha Usajili wa Jina la Biashara, Pendo Smith Mrema (kushoto) mara baada ya usajili wa papo kwa hapo katika banda la BRELA la maonesho ya Sabasaba kwenye Viwanja vya maonesho vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2020. Katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa (kushoto) alipotembelea banda la BRELA la maonesho ya Sabasaba kwenye Viwanja vya maonesho vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2020.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) akizungumza na mteja aliyefika katika banda la BRELA kwa ajili ya kupata huduma katika banda la BRELA la maonesho ya Sabasaba kwenye Viwanja vya maonesho vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2020. Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa (kulia)akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar, Maryam Jecha alipotembelea banda la BRELA la maonesho ya Sabasaba kwenye Viwanja vya maonesho vya Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2020.


Wateja mbalimbali waliofanyiwa sajili za hapo kwa hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...