Na.Ashura Mohamed - SIMIYU

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametaja sababu zilizomsukuma kuwania tena ubunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoa Simiyu baada ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15 kwa mafanikio makubwa huku akibainisha kuwa kazi ya kusaka maendeleo katika jimbo hilo bado haijakamilika.


Akizungumza nje ya Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kuteuliwa kugombea Jimbo la Kisesa, Waziri Mpina amekishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kumruhusu kuchukua fomu hiyo na kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kuendelea kumuunga mkono katika safari hiyo.

“Naamua kuchukua fomu ya kugombea Jimbo la Kisesa kwa sababu kazi ya kusaka maendeleo ya jimbo bado haijakamilika”alisema Waziri Mpina.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Charles Mazuri amesema hadi kufikia Julai 15 saa saba mchana jumla wa watia nia nafasi ya ubunge kwa Jimbo la Kisesa walikuwa wamefikia 9 akiwemo Waziri Mpina na Mbunge anayemaliza muda wake.

Mazuri amesema kwa upande wa jimbo la Meatu jumla ya wagombea 11 wamejitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho na kufanya idadi ya wagombea 20 wanaowania nafasi hiyo kwa majimbo yote mawili.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kumlipia fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kisesa Waziri Mpina wamesema wamesukumwa na hali hiyo kutokana na uchapakazi wa mbunge huyo na maandeleo makubwa aliyowapatia katika kipindi cha uongozi wake.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa CCM kutoka Kata ya Mwakisandu, Monica Mirega amesema wanamshukuru kwa maendeleo aliyowaletea huku wakiamua kumtuma tena.

“Ni kijana mchapakazi, mwadilifu na hachoki katika kazi za maendeleo kwa hiyo nawaomba wanachama wote tumpe tena kura zetu arudi kuchapa kazi” Monica


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (kushoto) akipokea fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu. kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Charles Dotto Mazuri leo Julai 15, 2020
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiwa nje ya Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Meatu akionesha fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kugombea ubunge Jimbo la Kisesa Meatu Mkoa Simiyu leo Julai 15, 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...