Na Janeth Raphael, Globu ya jamii
WAZIRI wa viwanda na biashara wa Zanzibar Balozi Amina Salum amewapongeza Marais wa Tanzania upande wa bara Rais Dk John Magufuli na kwa upande wa Zanzibar Rais Dk Ali Mohammed Shein kwa jitihada walizochukua kukabiliana na janga linaliokumba Dunia kwa sasa #COVIDー19

Balozi Amina amesema kuwa Tanzania imekua nchi ya mfano kwa majirani zake na Ulaya kwa ujumla kwa namna ambavyo Marais hawa walijitoa mhanga kwa kukataa kufungia wananchi wake ndani na kutoa Uhuru wa kuendelea na shughuli za kila siku za kujipatia kipato na kutunza familia zao.

Balozi Amina ameyazungumza hayo leo Julai 13, 2020 wakati akifunga maonyesho ya 44 ya kimataifa ya biashara yaliyokua yanaendelea katika viwanja vya Mwalimu nyerere jijini Dar es salaam

Aidha Waziri Amina  amempongeza Rais Magufuli kwa kuwezesha nchi kuingia  katika uchumi wa Kati na kusema kuwa,

" Hakika ni hatua kubwa Sana Tanzania tumepiga na kutuwezesha kuingia katika nchi zinazoendelea, hakika tinajivunia hilo" Waziri Amina

Waziri Amina amewapongeza waandaaji wa maonyesho hayo (TANTRED) kwa kuwezesha maonyesho hayo kufanyika ingawa nchi bado imegubikwa na taharuki ya ugonjwa wa corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...