Na Sabiha Khamis na Ali Issa – Maelezo .

Mwenyekiti wa chama cha (Alliance for Democratic Change) ADC Hamad Rashid Mohamed amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watamchagua kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao ataimarisha sekta ya elimu na kutoa huduma hiyo bure hadi kufika kiwango cha elimu ya juu.

Hayo ameyasema katika ofisi yao huko Mtopepo Wilaya ya Magharibi “A” wakati alipokuwa akichukua fomu ya kuombea ya urais kupitia chama hicho amesema pindipo atapata madaraka ya kuongoza nchi atahakikisha kuwa serikali yake inatoa huduma hiyo bila ya gharama yoyote kwa wananchi.

Amesema yeye ni mzalendo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar hivyo atafanya juhudi hiyo na kuhakikisha kwamba jambo hilo linafanikiwa mara tu baada ya kuingia madarakani.

“Pindipo nitapata ridhaa ya kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa rais wa Zanzibar nitahakikisha kuwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu wanaochukua degree ya kwanza watasoma bure bila ya gharama yoyote kulipia katika mtaala huo wa elimu”, alisema Mhe. Hamad Rashid.

Aidha Mhe. Hamad alieleza kuwa pia ataimarisha ujenga nyumba za maendeleo zenye ghorofa tatu mpaka nne kila wilaya ili kuepuka migogoro ya ardhi pamoja na kuharibu mazingira.

Hata hivyo amefahamisha kuwa atainua uchumi wa Zanzibar kwa kupitia kilimo na uvuvi wa kisasa ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo pamoja na kuwaunganisha walimu wa madrasa na serikali pamoja kutoa hati ya kusafiria, kitambulisho cha Mzanzibar na Uraia wa nchi mbili kwa lengo la kuleta maendeleo .

Nae Mkurugenzi Mipango Uchaguzi wa chama hicho Omar Albat Costatine amesema fursa ya ugombea Urais wa chama chao ipo wazi kwa yoyote yule mwanachama muhimu kuzingatia sheria ya chama na miongozo iliopo.

Aidha alisema mgombea yoyote yule anae chukua fomu ya urais kupitia chama hicho atalazimika kuwa na wadhamini 100 kwa kila mkoa .
 Mtia nia ya Uraisi wa Zanzibar kupitia chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani ) mkoba wenye fomu ya kugombea nafasi hiyo.
 Mkurugenzi mipango uchaguzi wachama cha ADC Taifa Omar Albet Constantine akimkabidhi fomu ya Uraisi mtia nia yakugombea Uraisi wa Zanzibar kwatiketi ya Chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed.
 
 PICHA NA FAUZIA MUSSA  /MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...