Na Mashaka Mhando, Tanga .

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepewa zawadi ya kitenge na fedha taslimu Sh.30,000 kwa ajili ya mshono kutokana na jitihada zake ambazo amekuwa akizifanya kwa wanawake wa Kata ya Mabawa jijini Tanga.

Zawadi hiyo imetolewa leo Julai 10,2020 na wanawake wa kata hiyo ya Mabawa Jijini Tanga,baada ya Waziri Ummy Mwalimu kufanya ziara ziara katika kata za Jiji hilo na baada ya kuzindua kazi za kwanza za upasuaji katika kituo cha Afya Mikanjuni, wanawake hao walitumia nafasi hiyo kumpa kitenge na fedha hizo kama ishara ya kutambua kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya.

Mmoja ya wanawake hao alimwambia Waziri Ummy Mwalimu kuwa wanafurahi na wanamuunga mkono katika kazi unazozifanya katika kulitumikia Taifa na maendeleo ya wilaya za Jiji la Tanga."Tunakupa zawadi hii ya kitenge na fedha kwa ajili ya mshono, iwe kumbukumbu yetu kwako."

Kabla Waziri Ummy hajasema neno lolote aliletwa mtoto wa kike ambaye amekuwa wa kwanza kufanyiwa operesheni katika kituo hicho cha afya ambaye amepewa jina la Ummy.

Hata hivyo Waziri amefanya ziara katika Wilaya ya Tanga, ambapo amezindua madarasa mapya katika Shule ya Sekondari Mnyanjani, kisha akazindua huduma ya upasuaji katika vituo vya Afya vitatu Mikanjuni, Ngamiani na Makorora. 
 
Aidha katika kituo cha Afya Mikanjuni mtoto wa kwanza aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji amepewa jina la Ummy kuonesha heshima na shukurani kwake kutokana na kazi nzuri anayoifanya katika wizara hiyo anayoiongoza.

Waziri Ummy kitendo cha kupewa zawadi hiyo ya kitenge na fedha kwa ajili ya kushona kitenge hicho yalimfanya ajifikiria kiasi cha nusura atokwe na machazi ya furaha. Wanawake hao wamemtaka Waziri Ummy nguo atakayoshona kutokana na kitenge hicho aivae siku anayokwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge.

Pamoja na hayo Waziri Ummy amezindua rasmi Zahanati ya kisasa ya Mabokweni na kisha akaweka jiwe la msingi la Zahanati ya Kiruku ambayo iko katika hatua za mwisho. Akizungunza na wananchi kwa nyakati tofauti Ummy Mwalim amemshukuru Rais John Magufuli kwa mapenzi yake makubwa kwa wananchi wa Tanga kwa kutoa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Amewataka wananchi wa Tanga, kuungana na kumpigia kura zote za ndiyo Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao.Kuhusu zawadi ambayo amepewa amesema "Asanteni sana wanawake wa Kata ya Mabawa kwa upendo wenu mkubwa kwangu, zawadi hii imekuja wakati muafaka, nimeipokea zawadi hii ya kitenge cha CCM kwa heshma na unyenyekevu mkubwa." 

Amesema ili kukipa thamani kitenge hicho atakishona na Mungu akimjalia ndicho atakachokivaa siku akienda kuchukua fomu ya ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini."Asante sana wanawake wa Jiji la Tanga kwa upendo wenu na ushirikiano mkubwa mnaonipatia. Mungu awabariki...Nawapenda sana." 

Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi Lupakisyo Kapange akizungumza kwa niaba ya CCM wa Kiruku amesema Rais Magufuli amefanya mengi katika Wilaya ya Tanga ambako kulikuwa na vituo vya afya vinne na sasa vipo saba, zanahati zilikuwa 19 na sasa zipo 24, barabara za lami zimetengenezwa za kutosha jijini Tanga.
Wanawake wa kata ya mabawa wakimkabidhi kitenge Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na pesa za mashono
Waziri Ummy akiwa amembeba wajina wake mtoto aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji katika kituo cha afya Mikanjuni,Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga Daud Mayeji




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...