Benki ya Maendeleo TIB inashiriki Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Benki ya Maendeleo ya TIB inashiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa umma, kutangaza huduma inayozitoa pamoja na kuvutia wateja wapya kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya kimkakati nchini.

Pia, benki inatumia fursa hiyo kutoa ushuhuda wa miradi ya kimikakati iliyokopeshwa kwa wateja wake waliotapakaa nchi nzima.
Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa TIB, Bw. Patrick Mongella (kushoto) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki hiyo kutoka Kampuni ya Mwasonge Farms, Bw. Walter Nyoni (kulia).
Baadhi ya wateja wa Benki ya Maendeleo TIB wanaoshiriki Maonesho ya Nane Nane wakionesha bidhaa wanazozizalisha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo TIB wakiwa tayari kuwahudumia wateja na wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...