Na Karama Kenyunko Michuzi TV.

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji ( NIT), kinatarajia kuanza kutoa kozi ya wasanifu na wajenzi wa meli kwa lengo la kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa juu ambapo mpaka sasa wameishaunda mitaala mbali mbali na sasa wanasubiri ithibati kutoka Necta ili  mwaka wa masomo 2020-2021 waweze kuanza masomo hayo.

Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zacharia Mganilwa ameyasema hayo leo Agosti 13, 2020 wakati ya ziara ya baraza la uongozi wa Chuo hicho katika Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kufuatia kuingiza mawazo ya TPA katika mitaala yao mipya.

Amesema, kabla ya kuanza kuitengeneza mitaala hiyo mipya ambayo imeishakamilika waliwashirikisha TPA ili wakianza kutoa kozi ziendane na mahitaji ya mamlaka hiyo na kuongeza rasilimali watu (wataalamu).

"Lengo kubwa la kuja hapa leo ni kuwaeleza kwamba mawazo yenu yote mliyoyatoa tumeyaingiza kwenye mitaala yetu mipya ambayo imeishakamilika na kuanzia Novemba tutaanza kudahili wanafunzi wapya wanaohusiana na upanuzi wa bandari," amesema Profesa Mganilwa

Amesema, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Bandari hiyo,  asilimia 50 ya wafanyakazi wa TPA ni wanafunzi kutoka NIT hivyo kutokana ma mradi huo wa upanuzi wa Bandari, mahitaji yao yataongezeka zaidi ndio maana katika ziara hiyo baraza la uongozi la Chuo odi imeshiriki ili wajue wanafunzi baada ya kumaliza wanakwenda wapi na pia wajue mahitaji muhimu ya wadau kama TPA ambao wanachangamoto.

Profesa Mganilwa ameongeza kuwa, lazima changamoto za TPA wazichukue wazibadilishe ziwe fursa, mfano, upanuzi wa bandari uendane na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano, haswa katika uchumi wa viwanda ambapo malighafi nyingi zitaagizwa kwa usafiri wa njianya maji na poa kusafirisha malighafi nyingi zaidi kuliko vilivyo hivi sasa kwa hiyo kutahitajika wataalamu wa kuendana na kasi ya uchumi wa viwanda.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa bandari ya Dar es Salaam, (TPA) Elihuruma Lema Amesema, ujio wa bodi ya NIT bandarini hapo unatarajiwa kufanikisha  uboreshaji wa Bandari kwa kujua namna ya kuanza kutoa mafunzo kwa wafanyakazi  katika maeneo yani kuendesha mitambo na kuitengeneza, maeneo ambayo yanamahitaji makubwa kila siku.

Tunatarajia tutafanya nao kazi kwa kiasi kikubwa na nadhani ipo haja ya kuingia mkataba wa makubaliano ili kuangalia ni jinsi gani tutakuwa tunawapa mafunzo wafanyakazi wa mamlaka ya Bandari kwa kutumia NIT ili kuongeza ufanisi wa bandari na kuendana na kazi ya upanuzi wa kina cha Bahari ambao unaendelea kufanyika", amesema Lema.

Ameongeza kuwa, maboresho yanayoendelea ya upanuzi wa Bandari yameongeza ufanisi mkubwa kutoka gati namba moja mpaka namba nne ambapo kwa sasa kuna meli kubwa ambazo awali zilipokuwa zikija zilikuwa zinatumia takribani Sik  12 na zaidi kushusha mzigo lakini baada ya maboresho haya meli kubwa zinatumia nusu ya siku walizokuwa wakitumia zamani kumaliza kuzusha mzigo.

 "Kwa sasa tumekuwa tukihudumia meli nyingi sana na idadi ya kupakua magari pia imeongezeka kwani Bandari inauwezo wa kupakua magari mengi zaidi ya hapo awali. Kwa kutumia muda mfupi",amesema.

Amesema, kwa sasa mizigo ya ina yote inaingia kwa wingi katika Bandari ya Dar es Salaam, tofauti na kwa kuangalia katika miaka miwili iliyopita na kuongeza kuwa serikali ya awamu ya tano imekuwa na mradi mingi ya ujenzi hivyo mizigo ya general cargo imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

"Ushirikiano wetu na NIT wa sasa ni tofauti na ule wa awali ambapo ulikuwa ni wa mmoja mmoja, yaani mfanyakazi mmoja mmoja anaenda anaomba likizo ama ruhusa anaenda kusoma NIT kisha anarudi, ambapo tumeweza kusomesha wafanyakazi wengi takribani asilimia 50. Lakini sasa baada ya ujio huu na kutakuwa na mabadiliko nanufanisi utaongezeka amesema Lema.

Naye, Rais wa serikali ya wanafunzi NIT  Abel Joseph amesema,  amefurahi kusikia kuwa watu ama nguvu kazinkytoka NIT inakidhi matakwa na unafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa TPA inazidi kukua

"Ninafuraha kubwa kuona kwamba wataalamu wanaozalishwa na Chuo chetu wanakichi matarajio ya viwanda na wanakidhi matarajio ya TPA,  hivyo katika upanuzi huu chini ya awamu ya tano ambayo inafanyikainafanyika NIT itaendelea kutoa wataalamu wakubwa zaidi katika sekta mbalimbali ili kusaidia katika sekta hii ya usafirishaji wa madini kuendelea kukua na kusaidia nchi yetu katika kukua kwa uchumi", amesema Rais huyo wa Chuo.

 Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Elihuruma Lema akiwaeleza uongozi wa Chuo cha NIT  hali ya ujenzi wa upanuzi wa Bandari unaoendelea kufanyika katika Bandari hiyo wakati wa ziara ya bodi ya Chuo hicho leo Agosti 12, 2020
 Mkuu wa Chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yao kwa kuangalia ujenzi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam unaoendelea leo Agosti 12,2020

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...