Na Pamela Mollel,Arusha.

Chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kimeendelea kutoa mafunzo ya biashara kwa vikundi vya wafugaji, wakulima na wasindikaji  katika Kipindi cha nanenane Arusha, ambapo wanawajengea uwezo ili waweze kufanya  shughuli zao kwa tija zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Chuo cha uhasibu Arusha,Prof Eliamani Sedokeya amesema kuwa pamoja na Mambo mengine chuo hicho kinaendelea kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali ili waweze kumudu soko vizuri

Pia amesema Chuo hicho kinaendelea kufanya udahili kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali zinazipatika chuoni hapo katika ngazi za Astashahada,Stashahada na Shahada ya uzamili

Ametaka wanafunzi na wadau wa elimu kuchangamkia fursa hiyo ya kuendelea kujiunga na chuo hicho yenye matawi yake Arusha,Babati na Dar es Saalam

Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kwa maendeleo ya kilimo,mifugo uvuvi chagua kiongozi bora 2020"

 Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha,Prof Eliamani Sedokeya akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya nane nane katika viwanja vya Taso Mkoani Arusha
 Mhadhiri wa chuo cha uhasibu Arusha Felix Mlay akitoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali
 Afisa Udahili Mr. Gerald Malisa akitoa elimu kwa makundi ya watu waliotembelea banda hilo

 Baada ya kupata mafunzo vikundi mbalimbali vilipatiwa vyeti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...