WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Maziwa cha Tanga Freshi Jijini Tanga kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Tanga Fresh Inocent Mushi kulia ni Mwenyekiti wa cha ushirika wa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa mkoa wa Tanga (TDCU) Hamid Mzee
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha Maziwa cha Tanga fresh Jijini Tanga .

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (TADB) Japhet Justine akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mtendaji Mkuu wa Tanga Fresh Inocent Mushi akitoa taarifa ya kiwanda hicho kwa Waziri Mpina ambaye amekaa kulia.
Mwenyekiti wa chama cha ushirika wa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa mkoa wa Tanga (TDCU) Hamid Mzee akieleza jambo wakati wa ziara hiyo
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema hakuna sababu ya kuagizwa maziwa kutoka nje ya nchi kutokana na uwepo wa mifugo ya kutosha ambayo ikiwekewa utaratibu mzuri itajitosheleza kuzalisha bidhaa hiyo kwa kiasi cha kutosha.


Mpina aliyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga aliyoambatana na watendaji mbalimbali.

Alisema kwani hivi sasa maziwa hapa nchini ni mengi kutokana na uwepo wa viwanda vya kuzalisha maziwa kwa njia ya mchakato ambavyo vimetakiwa kuzalisha kwa wingi na kukuza soko ili kukwepa uingizwaji wa maziwa kutoka nje ya nchi.

"Tumeweza kuona changamoto na fursa mlizonazo kuanzia kwenye mifugo mpaka uzalishaji na masoko, nawapongeza sana Tanga fresh kwasasa kwa kazi nzuri mnayofanya, hakuna sababu ya watu kuingiza maziwa kutoka nje ya nchi wakati tuna mifugo ya kutosha kutupatia maziwa" alisema Mpina.

Waziri Mpina aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kununua maziwa kwa wafugaji kwa bei itakayomfanya mfugaji kunufaika na uzalishaji wa mifugo yake hatua inayotokana na kutokuwepo kwa bei elekezi ya kununulia maziwa kwa mfugaji.

"Changamoto nyingine ni hii ya bei, tulipotangaza ununuzi wa maziwa hatukuweka bei elekezi lakini ningependa bei ya maziwa kwa mfugaji iwe ni shilingi mia nane kwa lita, nitafurahi na nitapenda kwa kila kiwanda kinunue maziwa kwa mfugaji kwa bei hiyo"
alibainisha.

Akifafanua kuhusu changamoto ya magonjwa kwa mifugo, Waziri Mpina alisema ili kupata maziwa kwa wingi na yenye ubora ipo haja ya kuangalia ukuaji wa mifugo hususani katika magonjwa, lishe na  chanjo pamoja na mazingira wanayoishi.

"Mkurugenzi wa nyanja za malisho muende muwatembelee wafugaji kule kwenye maeneo yao muone maeneo wanayofugia, vyakula wanavyoipatia mifugo na hata chanjo ili kuwakinga na
magonjwa" alisema Mpina.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa chama cha ushirika wa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa mkoa wa Tanga (TDCU) Hamid Mzee alisema changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wafugaji ni migogoro ya ardhi na kueleza kwamba wanatakiwa kuweka mpango mkakati ili kutengeneza maligafi kwa wingi na kukwepa ukosefu wa bidhaa hiyo.

Mwenyekiti huyo pia aliiomba serikali kuangalia kwa ukaribu wafugaji na kuwawezesha kuzalisha kwa tija huku wakinufaika na mifugo yao kwani tatizo la uzalishaji lililokuwepo awali kwa sasa limepungua na kufanya soko kuongezeka.

"Migogoro ya kunyang’ anyana ardhi ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita hatukuweza kuzalisha mitamba ya kutosha na kusababisha tatizo la kuoungua kwa uzalishaji lakini sasa soko limerudi tena, niiombe serikali ijitahidi kuliangalia hili suala ili wafugaji wetu wanufaike na mazao yao ya mifugo" Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema pia changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wafugaji ni migogoro ya ardhi na kueleza kwamba wanatakiwa kuweka mpango mkakati ili kutengeneza maligafi kwa wingi na kukwepa ukosefu wa bidhaa hiyo.

Mwenyekiti huyo pia aliiomba serikali kuangalia kwa ukaribu wafugaji na kuwawezesha kuzalisha kwa tija huku wakinufaika na mifugo yao kwani tatizo la uzalishaji lililokuwepo awali kwa sasa limepungua na kufanya soko kuongezeka.

"Migogoro ya kunyang’ anyana ardhi ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita hatukuweza kuzalisha mitamba ya kutosha na kusababisha tatizo la kuoungua kwa uzalishaji lakini sasa soko limerudi tena, niiombe serikali ijitahidi kuliangalia hili suala ili wafugaji wetu wanufaike na mazao yao ya mifugo" Alisema Mwenyekiti huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...