IMEELEZWA kuwa kwa mwaka 2020/2021  bei ya mbolea ya kupandia(DAP) kitaifa itauzwa kwa shilingi 55,573 kwa mfuko wa kilogramu 50 ikilinganishwa na msimu wa kilimo uliopita ambayo iliuzwa kwa shilingi 58,433.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
  
Kwa upande wa mbolea ya kukuzia (UREA) itauzwa kwa shilingi 48,070 kwa mfuko wa kilogramu 50 ikilinganishwa na shilingi 49386 ya msimu wa mwaka 2019/2020

''Kwa hiyo kuanzia leo,nikianzia na mbolea ya DAP   kwa mkoa wa Arusha itakua shilingi 55356 ikilinganishwa na shilingi 58208 ya mwaka jana ambapo itakua imepungua kwa shilingi 2852 kwa mfuko wa kilo 50,"alisema Waziri.

Alisema kwa mkoa wa Dodoma bei elekezi ni shilingi 53,925 ikilinganishwa na shilingi 56790  ya awali ambayo imepungua kwa shilingi 2,865.

Kwa Dar es salaam bei elekezi itakuwa shilingi 48717 ikilinganishwa na msimu uliopita 51952 itakuwa imepungua kwa shilingi 3235.

Geita bei elekezi itakuwa ni shilingi 58313 ikilinganishwa na bei ya mwaka jana 61138 itakuwa imepungua kwa shilingi 2825.

Kilimanjaro bei elekezi 54316 ikilinganishwa na 57178 ya msimu uliopita na hivyo itakuwa imepungua kwa shilingi 2816. 

Mkoa wa Mbeya bei elekezi itakuwa ni shilingi 59136 ikilinganishwa na bei iliyopita shilingi 59136 itakuwa imepungya kwa shilingi.

Mkoa wa Songwe bei elekezi ni shilingi 57480 ikilinganishwa na msimu uliopita shilingi 60318.

"Bei hizo ni bei elekezi za juu hivyo inatakiwa ieleweke kuwa hizo ndizo bei za juu labda huko kijijini sana inaweza ikapanda kidogo ambapo ukichukua kwa wastani Nchini nzima kwa ujumla mwaka jana bei elekezi ilikuwa ni shilingi 58433 na kwa mwaka huu bei mpya ninazozitangaza ni wastani wa shilingi 55573 ambapo ukichukua mkoa wa kagera ambao ndo mkoa ulio mbali bei elekezi 591195 ukilinganisha na bei iliyopita ambapo ilikuwa shilingi 62110,"

Alisema kuwa bei ya mbolea ya kupandia imeshuka amesema unafuu huo uongeze matumizi ya mbolea kufikia kiwango cha kimataifa kinachotakiwa lakini pia kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara na yale ya chakula hivyo nchi itakuwa na chakula cha kutosha.

Bei elekezi kwa aina ya pili ya mbolea ya kukuzia(UREA) kwa mfuko wa kilo50 Arusha bei elekezi itakuwa ni shilingi 47,698 ukilinganisha na bei ya msimu uliopita 48998,Dodoma bei elekezi itakuwa ni shilingi 46267 ukilinganisha na bei iliyopita ambayo ilikuwa ni shilingi 47633.
Na Geita ni shilingi 50,655 ukilinganisha na bei ya msimu uliopita ilikuwa ni shilingi 51820

Mbeya bei elekezi ni shilingi 48635 ukilinganisha na bei ya mwaka jana 49892 
Mikoa yote  mwaka jana wastani wa UREA ilikuwa 49386 na sasa 48070 ambapo imepungua kwa shilingi 1316.

Na bei elekezi kwa mbolea zilizoingizwa na vyama vya ushirika kwa msimu huu mfuko mmoja utakuwa ni shilingi Kwa DAP 50,000 kwa mfiko wa kilo 50.

Mbolea hiyo iwafikie wanachi palepale kwenye chama kwa bei hiyo,tofauti na wafanyabishara wengine wanaofikishia mikoani, kuhusu UREA alisema bei elekezi kwa vyama vya ushirika itakuwa ni 43500 kutakuwa na unafuu mkubwa sana na unafuu huu unatokana kwamba kama tungekuwa tunatumia vyama vya ushirika katika kuagiza mbolea hizi wakulima wangepata mbolea kwa bei ya chini sana.

Ameviagiza vyama vyote vya ushirika kutumia fulsa hii iliyopo na mazingira wezeshi yaliyotengenezwa na serikali ya awami ya tano kuhakikisha wanaagiza mbolea kwa pamoja ili waweze kuwahudumia wananchi wao vizuri.

Hata hivyo alisema kusingetokea maambukizi ya virusi vya  Corona Duniani bei hizo zingeshuka zaidi.

Pia alisema thamani ya shilingi nchini imeshuka na dola imepanda na hivyo gharama ya kubadilisha dola kuwa kubwa ikiwekwa kwenye shilingi ya Tanzania bei zinaongezeka zaidi.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma kuhusiana na bei mpya ya mbolea kwa Msimu mpya wa Kilimo wa 2020/21.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...